Maishafrika Adventure for the best Safari in East Africa

Thursday, January 7, 2016

UNAWEZAJE KUWA MJASIRIAMALI UKIWA UMEAJIRIWA

 
 
Hili swali limekuwa ni gumu na mtihani kwa watu wengi sana ambao ni waajiriwa wa sekta binafsi na wale walio ajiriwa kwenye mashirika ya umma. Na wengi wamekuwa wakipewa ushauri mbaya ama ushauri uliowakatisha tama. Leo ningependa kukwambia unaweza kuwa mjasiria mali bila kuacha kazi iliyokuwa ikikuingizia kipato kila mwezi. Una uwezo wa kuwa mjasiriamali na kuendelea kufurahia kazi unayoifanya kila siku bila kuaribu utaratibu wako wa kazi. Yafuatayo ni mambo matano muhimu yatakayokusaidia kufanikisha hili;
 
Ichukulie kazi yako kama ni Baraka kutoka kwa mungu.
kazi yako si mzigo mkubwa unaoubeba na unatamani siku moja uushushe. Kazi yako ndiyo inayokuwekea chakula mezani wewe na familia yako na pia ndiyo inayokufanya wewe kuheshimika katika jamii yako. Na pia kimbuka kazi yako ndiyo itakayokuwa muongozo ama mtaji wako katika biashara yoyote unayotegemea kuianzisha. Your job will make your entrepreneur dream come true. Mshahara wako utakuwa chanzo kikibwa cha wewe kuwa na nguvu ya kuchukua mkopo ama kuweka akiba ya kukuwezesha wewe kupata kianzio cha biashara ndogo unayotakiwa kuianzisha na si kuichukia ajira. Ajira yako ndiyo itakayo kunyanyua katika mipangilio yako yote ya ujasiria mali hadi pale utakapokuwa na mafanikio makubwa na una uwezo wa kuacha kazi na kusimamia biashara zako wewe mwenyewe. Kama biashara yako haijashamiri tafadhali epuka kuacha kazi na kwenda kusimamia biashara ambayo hujafahamu muelekeo wake.
 
Jali muda wako
Madhara ya kuwa kwenye ajira ukiwa ni mjasiriamali yapo na ni makubwa kiasi ambayo hukatisha tamaa watu wengi. Hilo lisikutishe wala kukusumbua, swala la muhimu ni kujipangia muda utakaofanya kazi na muda utakaotumia kwenye kazi zako za kijasiriamali. Jaribu kila muda unaoupata baada ya kazi unautumia katika kufanya shuguli zako za kijasiriamali. Sheria za kazi za umma ni kufanya kazi masaa nane ama tisa na katika sekta binafsi baadhi ni masaa hayohayo na mashirika mengina wanaongeza muda zaidi kwa makubaliano maalumu ama muda ni pungufu zaidi. Mara nyingi unapofanya kazi masaa tisa unakuwa na masaa si chini ya manne abla ya kulala ama kupumzisha mwili. Masaa manne ni muda mrefu sana kwa kusimamia kazi zako za ziada. Unaweza kuajiri mtu wa kuzifanya kazi hizo na wewe kutumia muda wako mchache kusimamia ama unaweza pia kuzifanya mwenyewe katika hayo masaa manne. Kwa mfano kilimo, unaweza kukifanya muda ambao upo nyumbani, ama ufugaji na biashara ndogondogo pia una uwezo wa kuzifanya mwenyewe kwa muda mfupi baada ya kazi. Ili kuwa mjasiriamali inabidi upunguze muda wa kufanya vitu ambavyo havikuingizii vipato na badala yake jaribu kufikiria na kujituma katika mambo yatakayokusaidia kukuingizia kipato cha ziada. Jaribu kuweka smart phone yako mbali na jaribu kuepuka kupoteza muda kwenye social media, jaribu pia kupunguza muda wa kulala na jiulize je muda ambao nipo free ninaweza kuutumiaje kujiongezea kipato. Kumbuka kila lisaa unalopoteza ni sawa na kupoteza kipato.
 
Chukua hatua kwa kila mpango ulionao.
Unapokuwa na malengo ya kuwa mjasiriamali ukiwa umeajiriwa, unatakiwa kuwa na malengo na kuhakikisha umefanikisha ndoto yako. Fikiria ni kitu gani kinaweza kukuongezea kipato na je mtaji wake utaupataje. Hili ni jambo la muhimu sana, hakikisha unafanya biashara ama shuguli itakayoendana na kipato chako na una uzoefu nayo na pia hakikisha unakuwa na uwezo wa kusimamia ipasavyo. Ni vigumusana kuanza biashara kubwa kuliko mtaji uliokuwa nao kwasababu biashara hiyo itakuwa ni ndoto isiyotimia. Hakikisha kama ni kuchukua mkopo, unachukua mkopo utakaoweza kuulipa na hata biashara itakapoenda vibaya ajira yako inaweza kulipa mkopo huo.
 
Ni kipi utakachokifanya tofauti na wenzako
Jaribu kufanya biashara tofauti na wenzako, usifanye biashara ambayo inafanana katika eneo moja. Na kama ni biashara inayofanana na wenzako hakikisha ya kwako una kitu tofauti na wanachokifanya wenzako. Hii itakusaidia kupata wateja wengi na mzunguka wa mtaji wako kwenda kwa haraka zaidi na kupelekea kipato chako kuongezeka kama ambavyo lilikuwa lengo la biashara.
 
 
Fanya ajira yako kuwa muongozo wa biashara yako
unapoamshwa na simu ama alarm clock asubuhi, usisikitike muda wa kazi umefika bali amka wahi kazini ili uwahi kutoka na kwenda kusimamia biashara zako. Kazi yako ndiyo ajira yako ya kwanza na biashara yako ndiyo ajira yako ya pili. Na usisahau ajira yako ndiyo muongozo wa biashara yako kwani ni moja ya kitu kinachokuongezea kipato ambacho ndiyo msingi wa biashara yako. Na kama ujasiriamali wako unaufanyia katika ofisi yako uliyoajiriwa tumia fursa vizuri bila kufaya uzembe wala kuvunja sharia za kazi na kuvuka mipaka ya kazi. Kumbuka ajira ni muhimu na ujasiria mali pia ni muhimu sana.

Sunday, January 3, 2016

JINSI YA KUWEZA KUWEKA AKIBA KILA MWEZI



Hii ni ya kufungia mwaka 2015, Mwaka 2016 ni mwaka wa kuhifadhi pesa na ni mwaka wa kufanya maendeleo. Kila mtu anapenda kufanya maendeleo na anatamani kuwa kama Fulani. Lakini kila unapojaribu kueka akiba inashindikana na wakati mwingine unajikuta umekuwa na matumizi makubwa kuliko ulivyotarajia na labda wakati mwingine umetumia fedha zaidi ya kipato chako cha kila mwezi bila kutegemea. Je ni jinsi gani unaweza kujiwekea akiba kila mwezi kutoka kwenye mshahara wako ama kipato chako cha kila mwezi.

Kabla ya kufikiria kujiwekea akiba angalia kipato chako kwa kila mwezi
Hii itakusaidia kujua ama kufahamu ni kiasi gani unatakiwa kuweka akiba na kama kipato chako kipo katika nafasi ya kuweza kuweka akiba. Baada ya kulifahamu  hili kuna mambo muhimu ya kufahamu katika kipato chako.


Madeni
Hakikisha umelipa madeni yako yote kabla hujafikiria kuanza kuweka akiba, hii ni kwasababu kila akiba utakayokuwa unaweka itakuwa si akiba tena bali ni fedha ya kulipia madeni.

Tengeneza Budget yako ya kila wiki ama kila mwezi
Ni lazima ujifunze kufahamu matumizi yako ya wiki ama ya mwezi.Hii itakusaidi kujua ni kiasi gani cha matumizi yako na hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha fedha unaweza kuweka akiba kila mwezi. Hii pia itakusaidia kujua kama matumizi yako yanaendana na kipato chako. Jaribu kuangalia katika matumizi yako kuna vitu ambavyo si vya muhimu unavyoweza kuvipunguza kwenye bajeti yako ama kuvitoa kabisa. Ni vizuri kama utatayarisha shopping listi yako ya wiki na ya mwezi katika kijitabu ili kujua matumizi yako ipasavyo. Epuka kula katika migahawa mara kwa mara na ujaribu pia kupunguza mitoko ya jioni kwasababu imeonekana chakula unachotengeneza nyumbani kinakusaidia kuokoa zaidi ya asilimia 50 ya fedha ya kununulia chakula. Jaribu pia kujali bei ya bidhaa na si kujali bidhaa ambazo ni bei gali na mengine mengi yatakayokusaidia kuweza kupunguza matumizi yasiyi ya lazima.

Jaribu kuandika mahali ndoto zako (Goals)
Ni lazima utambue your goals, hili litakusaidi kufahamu dhumuni la kutaka kuweka akiba. Kuna mtu anataka kuweka akiba ili anunue gari, mwingine ili anunue nyumba ama kiwanja na ajenge nyumba na mwingine labda anataka aweke akiba ili ampeleke mototo katika shule nzuri zaini na kadhalika. Malengo ni mengi na kuwa na malengo mengi na makubwa itakuwa vizuri zaidi ili kuwa na uwezo na kuhakikisha unabana matumizi zaidi ili kutimiza ndoto ama matarajio yako.


Ni muhimu pia kuhakikisha unaongeza njia zingine za kukupatia kipato ama kukuongezea kipato. Kama wewe ni umeajiriwa sehemu jaribu kufanya kitu kingine kitakachokuongezea kipato. Na kama wewe ni mjasiriamali jaribu kuongeza kipato unachokipata kwa sasa. Hili litakusaidia kuweka akiba kubwa zaidi kwasababu katika biashara ama kutafuta ajira nyingine ya kukuongezea kipato itakusaidia kuweka akiba zaidi kwasababu kipato chako kimeongezeka na matumizi yatabaki palepale.

Pia itakuwa ni muhimu sana kujaribu kuwa na account ya benki utakayo itumia kwa kuweka akiba yako tu na si kuweka kila kipato unachokipata. Kama ni mjasiriamali ama muajiriwa ni muhimu kutenganisha akaunti ya benki unayotumia kuhifadhi kipato chako na akounti utakayoitumia kuhifadhi akiba yako. na ni muhimu kujaribu kutotumia hiyo account kabisa.

Natumaini mtalifuatilia hili na ushauri huu kwa sababu naamini huu ni mwaka wa maendeleo na ni mwaka wa kuwa watu tofauti na tulivyokuwa kipindi cha nyuma. Happy new year 2016 na mungu awabariki.

Thursday, September 10, 2015

Things you do not know about me "Pauline Barnabas"


So many people judge me the way they see me and the way they want me to be. But there are so many things that people do not know about me because of one big reason. I have got very few close friends and l try to keep my personal life very private.
l always keep my private life because l am an independent woman and l am not scared to face life challenges. Some people think telling people about what you are facing in life helps because it release stress, but to me l feel like l am the only person who can sort out my problems. This is because l discovered that not everyone will like you, your worse enemy is your close friend and your close friend is your worse enemy.
 
I always have few friends because if you have many friends they will not give you time to be alone and do your own thing. l am a person who need a space and l need a person who understand me and give me a space, as l sometimes need to be alone. l believe l need to be me and to make me be me it needs a moment of being alone and think what l want in all steps in the life.
 
l am a person who do not need to know about how other people live, l always say it in non of my business to know what other people do. All in all l am a very nice person to nice people, if you do not like me for any reason l do not care. And the worse thing is, if l know you don't like me l even do not west  time l just leave like you do not existing in this world.
 
 





Monday, August 3, 2015

WALLET ZA WADADA PIA ZINAPATIKANA KWA BEI POA


Wallet hizi za ukweli zinapatikana My Arusha Collection kwa bei nafuu sana. Ni shilingi 20,000 tu na mzigo ni wa kutosha. Tunawakaribisha wote dukani kwetu.

Sunday, August 2, 2015

VITU VIZURI HIVYO!!!!

Raba nzuri zinapatikana Dukani kwetu kwa bei ya shilingi 35,000 tu. Kuna za lather nyeupe na brown na pia za jeans nyeusi na grey. Wasiliana nasi kwa namba 0763825409, tutakuletea pale ulipo kwa wakaxi wa arusha.




Tuesday, July 14, 2015

I AM HAPPY, AND FOR THAT , I MAKE NO APOLOGIES.

With me what you see is what you get. Yes call me naive, but l love life. I like to see the best in people, and when someone is nice to my face, l tend to believe them. 

l am also happy to say that everyone that l have met in my life, l have gained something from them,either negative or positive. l dont let anyones insecurities, emotions or opinions bother me. l know that if l am happy, thats all that matters to me. l ignore those who choose  to publish their opinions without actually talking to me. Have a blessed wadnesday wote.

Friday, July 10, 2015

THINGS THAT INDEPENDENT WOWAN DON'T DO

Kuwa strong, independent woman si rahisi kwani kuna changamoto nyingi sana.  Ila kifupi ni mwanamke kuwa strong na independent woman. Na ili kuwa strong na independen wowan kuna ambayo unatakiwa kuyafahamu. Nayo ni kama ifuatavyo; 
Strong and independent woman do not neglet their careers. Firstly independent woman have their careers always at the forefront of their lives.  Working hard is something everyone should do. Fanya kazi kwa bidii utaona matunda siku moja.

Independent woman dont fail to handle their own situations. Kitu kimoja cha muhimu zaidi ni kwamba independent woman always handle their own situations iwe ni mbaya ama nzuri.  lndependent woman ufunga mdomo pale anapokuwa na shida ama tatizo kwenye maisha yake badala ya kumueleza kila mtu. 

They do not over react to bad situations or mistakes. They do let the mistakes roll off their backs and to learn from their bad choice. 

They do not rise to the bait of haters. Maadui wapo wengi sana katika maeneo yetu tunayoishi. Lakini huna haja ya kushindana na adui yako. Unatakiwa kushindana naye kwa maendeleo na busara zaidi.

They dont stop learning. Unatakiwa kujifunza zaidi ya unachokijua kwenye taaluma yako.
They also dont let other people affect their confidence. Jipende vile ulivyo na usiruhusu mtu yeyote kukunyima confidence kwa jinsi muonekano wako ulivyo.

La mwisho na la muhimu manaishi maisha yao na hawafanyi kitu ili kumkomoa mtu bali wanafanya kile chenye manufaa kwao. Nawatakia siku njema wote

Thursday, July 9, 2015

BE PROUD OF WHO YOU ARE


Be yourself, hili ndo jambo la muhimu zaidi. kwasababu if you are not you, how can you be proud of yourself? pia usiwe kama watu wanavyotaka uwe just be yourself.
Kuwa na confidence on real achievements and strength. Jikubali na jifanyie angalizo kwa yale mazuri yako na mabaya pia. Hii itasaidia wewe kujitambua ni wapi unahitaji kubadilika. 

Kuwa na confidence, jaribu kupay attention to your strength, your accomplishment and your triumphs. Pia unatakiwa kuwa proud of yourself.  Dont be too proud though, it can easly be confused with arrogance if you show too much pride towards yourseldf.
Pia unatakiwa kuwa na marafiki wanaokupenda na kukuheshimu jinsi ulivyo. 
Jaribu pia ku ignore hateful or mean comments from others if its about how you are.  La mwisho na la muhimu sana ni kujaribu ku understand and accept that sometimes criticism is completely untrue.  Nawatakia siku njema nikisisitiza be proud of who you are but olny in a positive way.



Wednesday, July 8, 2015

HOW TO LIVE LIFE TO THE FULLEST.

Maana ya maisha yako ni kitu unacho creat day after day with your your own actions and thoughts. Kila wakati unatakiwa kujiuliza ni kitu gang unaweza kujifunza, na ni jinsi gani unaweza ku move forward na to stop yourself from blaming other people kama mambo hayataenda sawa kama ulivyotarajia. What living life to the fullest looks like is up to you. Haya yafuatayo yanaweza kukusaidia kuishi maisha yako; 

Tambua kwamba maisha ni safari ndefu, na si mwisho wa kila kitu.
Kuwa muwazi kwako we mwenye na kwa wenzako pia
Jifunze kujikubali wewe mwenyewe na watu wengine watakukubali
Tambua thamani yako
Kuwa tayari kukubali ahangamoto za maisha
Kuwa tayari kubadilika
Jali afya yako
Jifunze kujali mambo ya sasa na kusahau mambo yaliyopita. 


Nawatakia juma tano njema.



Monday, July 6, 2015

I HAVE GOT 100 REASONS TO LOVE MY JOB.

Naipenda sana kazi yangu kuliko kitu chochote,ina changamoto nyingi lakini ina rewards, na wafanyakazi wenzangu are awsome. Ninajifunza kila wakati kutoka kwa watu waliobobea kwenye utalii wa kimataifa. Na kwasababu hii nimekuwa na uhuru wa ku think outside the box and have all thoughts considered. Na kingine kinachonifurahisha ni kuwa na muda wa kufanya biashara zangu ndogo zinazo niongezea kipato zaidi na kunifanya mimi kuwa mimi na si mtu yeyote. Ninachoweza kusema ni kwamba, punde tunapomaliza vyuo vikuu tusifikirie kuolewa kwanza, tujdenge maisha yetu kwanza then tuwe na familia ambazo tutakuwa na uwezo wa kuzihudumia. kuolewa unaweza kuolewa ukiwa na umri wowote, ila fursa hairudi mara mbili hata siku moja. Wanawake tuamle na tusimame kwa miguu yetu miwili kwani tunaweza. Ushauri wangu mie ni hard work pays. Fanya kazi kwa bidii na utaona matunda. Nawapenda sana na muwe na juma tatu njema.




Monday, June 15, 2015

SHE IS ALWAYS IN MY FAVOURATE DRESSES

 

A very cute girl "Jordin Sparks" ndo jina lake hilo, always anavaaga my favourate dresses. Kila ninapokuwa na kamtoko ka uakika lazima nizame google na ni print one of her dresses nimpelekee fundi wangu anishonee kama yeye. Anavaa magauni ya heshima na yenye kukufanya uwe free, hasa kwa watu wenye miili kama yetu. Nikimaanisha kwa watu wenye miili mikubwa kidogo yani si watu wembamba.

 
 
 





Sunday, June 14, 2015

AFRICAN PRINT FREE DRESSES

 

Ni kigauni kizuri na very Simple hasa week end ukiwa na kamtoko kako ka kwenda kupumzika mahali ukipata bia yako Bariiidi. Kama si mnywaji basi unaweza kujipatia soda ama kinywaji chochote kisicho na pombe. Hii ni kwa wale wadada wanaoenda na wakari tu. Niwatakie jumapili njema

 
 




Wednesday, June 10, 2015

HARD WORKING WOMEN HOLIDAY

Watu wengi wamekuwa wakiniuliza unajuaje kwamba mtu ni hard working? ki ufupi tu mtu hard working ni yue anaefanya kazi kwa bidii zote na si lazima iwe kazi ya kuajiriwa tu hata kujiajiri mwenyewe ni part of it. Na kama ni mtu unaejiweza ni vizuri pia ukiwa kama muajiriwa wa mahala Fulani haitoshi hiyo peke yake bai ni vizuri kama unaweza kujiongeza. Nikisema kujiongeza namaanisha kuto kutegemea ajira tu bali kujaribu pia kuwa mjasiriamali pia hata kama ni kabiashara kadogo ni bora kuliko kutokuwa nayo kabisa. Pamoja na kuwa na yote hayo ni vizuri pia mwanamke chapakazi uwe ni mtu unaejua ku Save ama kwa Kiswahili sanifu uwe unajua kuweka akiba pia. Manake si kila siku ni siku ya asali, kuna kipindi mambo yanaweza kubadilika gafla na kama ni mtu wa kujiwekea akiba basi mambo yako yatakuendea poa na hakuna atakaejua mambo yako si poa. Kwahiyo basi mwanamkw unatakiwa kuwa chapakazi ama kitaalamu zaidi wanasema (Hard working woman), ujue kujiongeza, kujiwekea akiba, na pia usijibane sana ni lazima ujipe raha ama nene? Next time ntakuja na topic moja nzuri sana ya jinsi ya kuwa muajiriwa na mjasiria mali at the same time. SO MSIONE KAMA NAKULA BATA SANA, NAJUA PIA KUZITAFUTA NA NDO MAANA NAJUA KUZITUMIA PIA. See you next time.

 








Thursday, May 14, 2015

PENDEZA KWA BEI POA















Pata bangili kwa bei poa sana ni pale pale My Arusha Collection. Piga simu namba 0763825409