JINSI YA KUCHAGUA KUWA NA FURAHA MAISHANI MWAKO
Katika maisha yako ni wewe tu ndiye utakae chagua kuwa na furaha. Kuwa na furaha ama kutokuwa na furaha ni chaguo lako. Kwa kila wakati utakaokuwa una hasira ama kukasirika unapoteza sekunde 60 ya furaha. Kuwa na furaha wakati wote, na kama watu hawataki kukuona na furaha, usiwajali. Maisha si ya kumnyenyekea kila mtu.
Kama unauwezo wa kujijua kama unaogopa, unafurahi , una unwezo wa kusimama na kuongea lolote hata kama sauti yako inaonyesha uoga, kujiamini na kuomba msaada pale unapo hitaji, na ujasiri wa kukubali msaada pale unapouhitaji, bila shaka una kila sababu ya kuwa ni mtu mwenye furaha kila wakati.
Simama leo hii na chukua maaumuzi ya kuwa ni mtu mwenye furaha
Chagua kuwa bora kuliko unavyodhani
Jipe nafasi ya kufanya kila unachoweza, Kuwa na malengo ya maisha yako na hakikisha unakuwa commited kuhakikisha unatimiza malengo yako bila kuruhusu changamoto zozote. Epuka kufananisha maisha yako na ya mtu yeyote. Kujiwekea malengo (Goals) na kutimiza malengo yako ni kati ya vitu vitakavyokufanya uwe na furaha. Hii itakuonyesha kwamba wewe ni mtu ambaye una malengo na una uwezo wa kutimiza malengo yako kwa wakati muafaka. Ila swala la muhimu zaidi ni kuepuka kujaribu kuwa kama mtu Fulani, ila usiache kujaribu kuwa zaidi ya watu wanavyofikiri. Na kama unataka kufanana na mtu jaribu kujifananisha na wewe mwenyewe ulivyokuwa kabla ya hapo ulipo. Wewe mwenyewe ndiyo mfano wako na siku zako utakuwa wewe na si mtu mwingine.
Chagua kuwa na marafiki ama watu wenye mwenenda mwema
Jaribu kutumia muda wako kuwa na marafiki ama watu wema na wenye busara. Marafiki ama mahusiano ya aina yoyote yanatakiwa kukusaidia na si kukuumiza. Kuwa na marafiki ama mahusiano na watu watakaokusaidia kutimiza malengo yako. Chagua marafiki watakaokufanya ufurahi kwa kuwajua na si kujuta kuwafahamu. Life is too short to spend time with people who suck the happiness out of you. Utakapojitoa kwenye urafiki na watu wasiofaa, itakusaidia kutambua kwamba unastahili kuishi maisha yako, na kuishi maisha yako ndiyo maisha ya kweli.
Focus na kile ulicho nacho, na si kile usichonacho
Unaposhukuru kwa kile ulichonacho unaonyesha kwamba hata kile kidogo ulichonacho kina thamani. hii itakusaidia kuwa ni mtu mwenye furaha, kwasababu umeridhika na kile ulichonacho na huta sononeka kwasababu mtu Fulani anacho na wewe huna. Lazima umshukuru mungu kwa kile alichokupa kwasababu kuna wengine walitaka kufika ulipofika lakini hawakuweza kwasababu tofauti.
Chagua kuwa na tabia nzuri
Kinachosababisha wakati mwingine kutokuwa na furaha ni kuwa na picha Fulani kwenye vichwa vyetu.Na sababu kubwa inayosababisha wengi wetu kukata tama ni kuangalia umbali tunaotaka kwenda badala ya kuangali tulipotoka. Kumbuka maisha ni safari ndefu sana na si makao kamili. Kila kinachotokea katika maisha ya kila siku ni zawadi na ni opportunity ya maisha. Kubaliana na yaliyotokea, tabasamu na likubali kama lilivyo. Ukikubali kwamba yaliyojiri leo ni bora then maisha yako yatakuwa bora kila siku. Siku zote tabia nzuri huleta matokeo mazuri.
Tabasamu kila wakati
Kutabasamu ni chaguo lako, na si miujiza. Usisubiri watu watabasamu, watu wanatakiwa kujifunza kutoka kwako jinsi ya kutabasamu.Tabasamu lako linaweza kufanya watu wa karibu yako kutabasamu pia. Tabasamu lako dogo kawaida hutuma ujumbe kwenye ubongo wako kwamba una furaha. Kwa wewe kutabasamu kila wakati kuna kufanya uwe ni mtu mwenye furaha.
Kuwa muwazi
Jaribu kuwa muwazi kwako mwenyewe na kwa kila mtu. Usiwe muongo na usie aminika bali kuwa muaminifu na mkarimu, fanya matendo mazuri na hii inapunguza ugumu wa kuishi na watu na maisha yako mwenyewe. unapovunja sharia ama masharti Fulani inakaribisha changamoto nyingi katika maisha yako ya kila siku. Fanya maisha yako kuwa simple sana na enjoy kila unachokifanya ambacho kiko sawa. Jaribu kuepuka drama zitakazo sababisha matatizo na madhara katika maisha yako.
Toa masaada pale inapowezekana
Jali watu, katika maisha utalipwa kwa yale mema uliyoyafanya. Unapotoa msaada kwa mtu anaehitaji msaada, mungu anakubariki katika maisha yako pia. Jaribu kufanya kitu kilicho juu ya uwezo wako, hasa katika kutoa msaada kutamfanya unaempa msaada afurahi na wewe kupunguza matatizo pia. Makosa makubwa tunayoyafanya ni kutoa misaada kwa watu wasiohitaji misaada na badala ya kuwasaidia tunawafanya wawe wavivu wa kazi na wavivu wa kufikiria. Fanya uchunguzi n a utatambua watu wanaotoa msaada kwa wasiohitaji msaada hufanya hivyo ili waonekane na watu wengine, ama ufanya hivyo ili kumkomoa mtu mwingine. Badala ya mambo yao huwa magumu kwasababu mungu hajatambua wala hajaona faida ya msaada aliotoa. Tunatakiwa kujifunza kufanya jambo pale ambapo kuna uhitaji mkubwa.
Inapofikia wakati wa kuachana, usifikirie marambili ila fanya maamuzi sahihi
Wakati mwingine unatakiwa kuwa na msimamo na maamuzi ya maisha yako. Upendo unadhamani lakini si kwa ugomvi ama mapambano, na usikubali wewe kugombana kwasababu ya upendo ama mapenzi. Tambua kuwa si sawa wewe kuwa unapambana juu ya mapenzi, bali na wewe unatakiwa kugombaniwa pia. Kama hawaoni umuhimu wa upendo wako ama mapenzi yako unatakiwa kuachana naye (Move on) na kutambua uliwapenda zaidi ya wao walivyokupenda . Baadhi ya mahusiano na changamoto zake ni fundisho na hatua tosha katika maisha. Ukilazimisha kuwa na mpenzi ama kupenda mtu asiyekupenda mambo yako yatakuwa mabaya zaidi kwasababu utakosa furaha. Jaribu kuachana na watu wasiothamini pendo lako ni hilo litakufanya uwe na furaha zaidi.
Kuwa tayari kuvuka hatua nyingine katika maisha
Una chaguo la kuendelea kushikilia vikwazo katika maisha yako ama, kuachana na vitu vilivyokukwaza ili uwe ni mtu mwenye furaha. Usikubali mafanikio yakuumize kichwa na kutokuwa na mafanikio kuumize moyo wako. Kila kunapokucha ni siku mpya na ni mwisho wa siku iliyopita, likubali hilo na fanya kazi kwa bidii, tabasamu, na angalia mbele na si kuangalia jana ulishindwa wapi. Na usisahau kutabasamu hakumaanishi kila wakati una furaha, bali wakati mwingine ina maana rahisi, kuwa wewe ni shupavu na uko tayari kukabiliana na changamoto za kimaisha.
Na kumbuka, akili yako ni hifadhi yako binafsi, usiruhusu imani potofu unayoambiwa na watu wanaokuzunguka. Ngozi yako ndiyo mipaka ya maisha yako, usikubali mtu yeyote kuingia ndani yake. Linda na heshimu mipaka yako na yale unayokubali kuambiwa ama kufanyiwa na watu. You are a role model of your self, uhitaji kufanana na mtu mwingine kwasababu wewe ni wewe na hakuna anayefanana na wewe.
Usiruhusu mawazo ya mtu yoyote yakufanye ubadilishe maisha yako na kubadilisha nmuonekano wako. Usijitoe kafara kwa vile ulivyo kwa kuwa mtu mwingine anakutoa kasoro. Jipende kama ulivyo ndani na nje. Hakuna mwenye nguvu ya kukufanya wewe ujione huna thamani, labda kama wewe mwenyewe utaruhusu hilo.
Chaguo ni lako, chagua kuwa na furaha.
No comments:
Post a Comment