Sunday, January 3, 2016
JINSI YA KUWEZA KUWEKA AKIBA KILA MWEZI
Hii ni ya kufungia mwaka 2015, Mwaka 2016 ni mwaka wa kuhifadhi pesa na ni mwaka wa kufanya maendeleo. Kila mtu anapenda kufanya maendeleo na anatamani kuwa kama Fulani. Lakini kila unapojaribu kueka akiba inashindikana na wakati mwingine unajikuta umekuwa na matumizi makubwa kuliko ulivyotarajia na labda wakati mwingine umetumia fedha zaidi ya kipato chako cha kila mwezi bila kutegemea. Je ni jinsi gani unaweza kujiwekea akiba kila mwezi kutoka kwenye mshahara wako ama kipato chako cha kila mwezi.
Kabla ya kufikiria kujiwekea akiba angalia kipato chako kwa kila mwezi
Hii itakusaidia kujua ama kufahamu ni kiasi gani unatakiwa kuweka akiba na kama kipato chako kipo katika nafasi ya kuweza kuweka akiba. Baada ya kulifahamu hili kuna mambo muhimu ya kufahamu katika kipato chako.
Madeni
Hakikisha umelipa madeni yako yote kabla hujafikiria kuanza kuweka akiba, hii ni kwasababu kila akiba utakayokuwa unaweka itakuwa si akiba tena bali ni fedha ya kulipia madeni.
Tengeneza Budget yako ya kila wiki ama kila mwezi
Ni lazima ujifunze kufahamu matumizi yako ya wiki ama ya mwezi.Hii itakusaidi kujua ni kiasi gani cha matumizi yako na hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha fedha unaweza kuweka akiba kila mwezi. Hii pia itakusaidia kujua kama matumizi yako yanaendana na kipato chako. Jaribu kuangalia katika matumizi yako kuna vitu ambavyo si vya muhimu unavyoweza kuvipunguza kwenye bajeti yako ama kuvitoa kabisa. Ni vizuri kama utatayarisha shopping listi yako ya wiki na ya mwezi katika kijitabu ili kujua matumizi yako ipasavyo. Epuka kula katika migahawa mara kwa mara na ujaribu pia kupunguza mitoko ya jioni kwasababu imeonekana chakula unachotengeneza nyumbani kinakusaidia kuokoa zaidi ya asilimia 50 ya fedha ya kununulia chakula. Jaribu pia kujali bei ya bidhaa na si kujali bidhaa ambazo ni bei gali na mengine mengi yatakayokusaidia kuweza kupunguza matumizi yasiyi ya lazima.
Jaribu kuandika mahali ndoto zako (Goals)
Ni lazima utambue your goals, hili litakusaidi kufahamu dhumuni la kutaka kuweka akiba. Kuna mtu anataka kuweka akiba ili anunue gari, mwingine ili anunue nyumba ama kiwanja na ajenge nyumba na mwingine labda anataka aweke akiba ili ampeleke mototo katika shule nzuri zaini na kadhalika. Malengo ni mengi na kuwa na malengo mengi na makubwa itakuwa vizuri zaidi ili kuwa na uwezo na kuhakikisha unabana matumizi zaidi ili kutimiza ndoto ama matarajio yako.
Ni muhimu pia kuhakikisha unaongeza njia zingine za kukupatia kipato ama kukuongezea kipato. Kama wewe ni umeajiriwa sehemu jaribu kufanya kitu kingine kitakachokuongezea kipato. Na kama wewe ni mjasiriamali jaribu kuongeza kipato unachokipata kwa sasa. Hili litakusaidia kuweka akiba kubwa zaidi kwasababu katika biashara ama kutafuta ajira nyingine ya kukuongezea kipato itakusaidia kuweka akiba zaidi kwasababu kipato chako kimeongezeka na matumizi yatabaki palepale.
Pia itakuwa ni muhimu sana kujaribu kuwa na account ya benki utakayo itumia kwa kuweka akiba yako tu na si kuweka kila kipato unachokipata. Kama ni mjasiriamali ama muajiriwa ni muhimu kutenganisha akaunti ya benki unayotumia kuhifadhi kipato chako na akounti utakayoitumia kuhifadhi akiba yako. na ni muhimu kujaribu kutotumia hiyo account kabisa.
Natumaini mtalifuatilia hili na ushauri huu kwa sababu naamini huu ni mwaka wa maendeleo na ni mwaka wa kuwa watu tofauti na tulivyokuwa kipindi cha nyuma. Happy new year 2016 na mungu awabariki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment