Glass ama vikombe vilivyo vunjika ama (chipped)? Usivitupe vina kazi nzuri sana, fuatana name hapa kwenye blogu hii nikufahamishe.
Nilikuwa nikikasirika sana ninapoona glasi na vikombe vyangu nilivyokuwa navipenda nikivivunja ama kumeguka mara kwa mara na nilishindwa kuvitumia tena japo nilikuwa nikivipenda sana. Jambo hili limekuwa likinisumbua sana hasa kipindi cha miezi ya karibuni kwani nilijikuta nikivunja vyombo karibu kila siku. Nimejikuta kwa mwezi najaza ndoo ya takataka vyombo vilivyovunjika. Ndipo nilipotafuta njia ya kutumia vikombe ama glasi zangu zilizomeguka tena kwasababu nilikuwa nazipenda sana na ilikuwa ngumu kuzitupa kwani nilijua sitaziona tena. Hiki ndicho kilichao nifanya nitumie glasi hizo na vikombe kupanda maua ama kupanda viungo vya chakula.
Hakikisha unakusanya vikombe na glasi zilizomeguka, Tafuta maua madogo yasiyokuwa na mizizi mikubwa ama kuhitajo nafasi kubwa kukua. Jaza udongo wenye mbole kwenye vikombe ama glasi na hakikisha unaweka mawe modogomadogo juu ya udingo ili ikusaidie kunyonya maji kwenye udongo kwani ukumbuke glasi ama kikombe hakina nafasi ya kupitisha maji kwa chini.
Mbanda mbegu zako ama panda miche ya maua ama viungo vya chakula. Kwangu mimi nilipanda maua yasiyo na mizizi mikubwa na nilipanda pia viungo kama giligilani, lettuce na green onions. Kwa kufanya hivi ilinipunguzia garama ya kununua giligilani na green onions kwakuwa nimekuwa nikizipata nyumbani kwangu baada ya kupanda kwenye kikombe. Na kwa wakati huo huo nyumba yangu una kuonekano mzuri sana kwakuwa kuna maua mazuri kwa muonekano tofauti.
Na pia nimekuwa nikiridhika pale ninapokiona kikombe change nilichokuwa nikikipenda ninakitumia tena kwa kuremba nyumba yangu. Tunatakiwa kutengeneza mazingira kwa kuepuka kutupa taka ngumu hovyo na kuhakikisha tunatafuta matumizi ya vyombo vilivyovunjika ambayo yatakuwa na faida wakati huohuo. Vikombe ama glasi hizi unaweza kupiga rangi ama kuremba kwa kuweka ribbon ili kuwa na muonekano mzuri ila kama ni mtu wa kupenda kuchagua vyombo vizuri basi muonekano tu wa kikombe ama glasi yako unatosha.
Hii ni desert au ice cream glass iliyomeguka ambayo imetumika kupanda ua zuri. Na glasi hii unaweza kuiweka ndani ama barazani na ikapendezesha nyumba.
Hii ni glass ya maji iliyopata mpasuko (crake) ambayo imetumika pia kupanda uwa na linaweza kukaamahali popote kama urembo.
Hizi ni aina tofauti za vikombe vilivyomeguka na visosa vyake vilivyotumika kupanda mauwa na vimpendeza sana na kuvutia
Hizi ni glazi za maji za ukubwa tofauti zilizotumika kupanda mauwa ya aina moja, japo unaweza pia kupanda mauwa ya aina tofauti.
Hii pia ni glasi iliyotumika kupanda maua ya aina tofauti ila ni mauwa yenye mizizi midogo na haiitaji nafasi kubwa.
Hizi ni birika za chai ama maziwa zilizotumika kupanda maua ya aina tofauti na pia mauwa kama haya yanaweza pia kupambwa kwenye meza ya sebuleni (coffee table) ama meza ya chakula (dining table)
Hiki ni kikombe cha kahawa kilichotumika kupanda viungo vya kupikia na hii unaweza kuviweka pia jikoni mwako kwani vinahitaji mwanga mdogo.
hii ni chupa ya asali iliyokwisha kutumika ambayo imetumika kupansa uwa dogo. Na kwa kuremba chupa kama hii ambayo ina muonekano kabisa wa chupa unaweza kufunga kamba ya riboni ama kamba ya gunia safi na ikaonekana kuwa tofauti na kamba zingine.
Hiki ni kikombe cha chai kilichotumika kupanda uwa aina ya aloe vera ndogo na kama inavyookekana imekuwa na muonekano mzuri sana.
Haya ni matayarisho ya vikombe vilivyomeguka nikivitayarisha kwa kupanda viungo vya chakula.
Hizi ni glasi za mvinyo za aina tofauti nilizozitumia kupanda maua madogo na kuweka mawe madogi kwa juu.
Hivi ni vikombe vya chai vilivyotumika kupanda maua vikiwa katika muonekano mzuri.
SAFI
ReplyDelete