Tumekuwa na mazoea ya kutupa chupa za mvinyo (wine) kila baada ya matumizi ya kinywaji hiki. Chupa hizi zinaweza kuwa na faida kubwa na pia kuwa na matumizi mbalimbali. Ni muhimu kuhifadhi mazingira kwa kujaribu kubadilisha matumizi ya chupa za mvinyo kwa kuzifanyia kazi tofauti kama kuremba na kupendezesha nyumba na maeneo tunayoishi.
unaweza kubadilisha matumizi ya chupa za mvinyo kama chungu cha kurembea maua (Flower verse) ama unaweza pia kutengeneza urembo mwingine wa kupendezesha nyumba yako. Unaweza kuchukua chupa ya wine iliyokwisha kutumika, ukaisafisha vizuri na kuipaka rangi unayopenda na hatimaye ikawa flower verse nzuri itakayopendezesha nyumba yako. Chupa hizi una uwezo wa kuiweka ndani ama nje ya nyumba yako.
Ni vizuri tuwe tunajaribu kutumia fursa kila tunapozipata, kwani hii si fursa ya kuremba nyumba tu ila inaweza kutumika kukuingizia kipato. Hii itakusaidia kuwa mjuzi zaidi na kujaribu kujifunza jinsi ya kuweza kutengeneza chupa hizi kwa ustadi zaidi.
Tunatakiwa kila wakati tuwe tunatafuta mawazo na uvumbuzi mpya, mawazo mapya, na kufikiri zaidi. Lakini kufikiria zaidi sio kufanya ama kutengeneza mambo mapya bali ni kujaribu kuishi kwa kuboresha mazingira kwa kubadilisha matumizi ya vitu ama bidhaa zilizokwisha kutumika ili kuweka mazingira safi kwa kuhakikisha bidhaa hizi zinatumika tena kama mpya. Tukiangalia sana kwenye mapambo ya nyumba utumiaji wa vitu vilivyotumika ni wa muhimu sana.
Na hii imesaidia badala ya kutupa chupa za mvinyo zilizokwisha kutumika tunazitumia kama mapambo ya nyumba. Chupa za wine zinaweza kudizainiwa na kubadilisha matumizi kwa kuzifanya kuwa urembo mahiri na tofauti nyumbani kwako. Chupa za mvinyo zinaweza kutumika kama flower verse, chungu cha maua na aina nyingine ya mapambo yanayoweza kufanya nyumba yako iwe na muonekano tofauti.
Kwa picha zilizopo hapa ninakuonyesha matumizi tofauti ya chupa za mvinyo zilizokwisha kutumika na jinsi gani unaweza kuzibadilisha na kuwa urembo nyumbani kwako. Njia zote za kuzipamba chupa hizi ni rahisi na pia hazina garama kubwa.
utahitaji baadhi ya vifaa katika urembaji wa chupa hizi, kama rangi za kusprey na si rangi za kupaka kwa mkono, gundi, kamba, inborn, na vifaa vingine kama mkasi n.k. hakikisha unasiku nzima ya kutosha na pia vifaa vingine unavyoviitaji utavijua pindi utakapokuwa tayari kwa kazi hii. Furahia kushinda ukiwa unafanya kazi na chupa za wine zilizokwisha kutumika.
Chupa hizi ni chupa za wine zilizokwisha kutumika, zikasafishwa vizuri na kutolewa lebo na kasha kupuliziwa rangi ya dhahabu ya kawaida, na hatimae zikapakwa urembo wa dhahabu katikati na chupa nyingine kupakwa juu. Zoezi hili ni rahisi na linachukua chini ya masaa mawili.Chupa hii inaweza kutumika kama flower verse nyumbani kwako ama kwenye sherehe yoyote. Zina muonekano wa kupendeza na kuvutia sana.
Unaweza pia kupuliza rangi ya silver kwenye chupa zako na rangi hiyo iwe ni rangi nyororo na pindi itakapokuwa imekauka vizuri paka kwa mkono rangi ya urembo wa silver ili chupa zako ziwe na muonekano mzuri. Epuka kupaka rangi tofauti ya urembo kwani chupa yako haitakuwa na muonekano mzuri. Chupa hizi unaweza kutumia kama flower verse ama kuzitumia kama urembo ndani ya nyumba yako.
Unaweza pia kupaka kila chupa na rangi tofauti, chupa hizi zilipakwa rangi ya kupuliza kwanza na hatimaye ilipakwa rangi ya urembo kwa juu ili kufanya rangi ya urembo kuwa imara zaidi na yenye muonekano wa kuvutia.
Hizi ni chupa za wine tofauti kwa ukubwa na upana, hapa ilitumika gundi na kamba nyembamba za rangi tofauti. Chupa hizi zilipakwa gundi ya maji (super glue haifai) na kuzungushwa kamba kwa ustadi mkubwa. Subiri hadi chupa ikauke vizuri na zitakuwa urombo mzuri wa ndani utakaopendezesha nyumba yako. Unaweza pia kubandika vifungo vya nguo za zamani ili kuongeza nakshi za chupa yako ama kuongezea kwa kutengeneza maua madogo ya nguo za zamani na kubandika na gundi juu ya kamba nyembamba juu ya chupa yako.
Watu wengi wamekuwa wakitumia mishumaa na kuweka ama kwenye kisosa au kununua mbao za kuweka mishumaa pale inapotumika ambapo huwa ni garama kubwa sana. Chupa za wine za ukubwa mbali mbali zinaweza kutumika ila hakikisha ni chupa iliyo na rangi moja na hakikisha unatoa lebo za kila chupa na chupa ibaki kama inavyoonekana kwenye picha. Utumiaji wa chupa hizi kwa matumizi ya mishumaa inafaa pale unapohitaji kutumia mishumaa mingi na si michache. Hii inaababisha mwanga wa mishumaa kufanya chupa zionekani na rangi tofauti na za kuvutia hasa nyakati za usiku.
Chupa za mvinyo zilizokwisha kutumika zinaweza pia kutumika katika bustani yako ya maua. Hii inasaidia bustani yako kuwa tofauti na ya kuvutia. Hii inapunguza matumizi ya mawe ama cement kuweka kingo za bustani yako ya maua. Huku ni kulinda mazingira na pia kupendezesha nyumba yako.
Chupa hizi za wine zinaweza pia kutumika kama flower verse kwenye garden yako na kwa garama nafuu tu. Chupa hizi kwenye picha zimesafisha ka kufungwa ama kuzungushiwa kitambaa nadhifu na kuwekwa maua na zinaonekana kuwa na muonekano mzuri sana. Unaweza kubadiliha aina ya vitambaa kutokana na zile rangi unazozipenda.
Kuremba na kupendezesha nyumba yako ni swala la muhimu na lakuvutia na haswa pale unapolinda mazingira. Natumai umejifunza kitu na kama utakuwa na swali ama wazo dondosha comment yako hapo na nitakujibu kwa muda muafaka.
Gundi YA aina gani inafaaa kutumika...YA maji BUT ni ipi specifically...pls help
ReplyDeleteGundi YA aina gani inafaaa kutumika...YA maji BUT ni ipi specifically...pls help
ReplyDeleteGundi YA aina gani inafaaa kutumika...YA maji BUT ni ipi specifically...pls help
ReplyDeleteGundi YA aina gani inafaaa kutumika...YA maji BUT ni ipi specifically...pls help
ReplyDeleteMahitaj kujua fundi ya maji ni ipi na jina lake??
ReplyDeleteMimi ninazo chupa mnanunua pesa
ReplyDelete