Maishafrika Adventure for the best Safari in East Africa

Thursday, March 16, 2017

JINSI YA KUKUZA VIUNGO NDANI YA NYUMBA (Indoor Herb Garden)




Baadhi ya herbs unazoweza kupanda ndani ya nyumba yako


Baadhi ya Herbs zilizopandwa ndani ya nyumba kwa kutumia makopo ya plastic yaliyokwisha kutumika na kupakwa rangi monja

Upandaji wa Herbs kwa matumizi kama viungo na kutumika kama urembo wakati huo huo



Vikombe maalum vilivyotumika kupanda Herbs na kuandikwa aina ya herbs ili kufanya urahisi wa kutambua aina ya kiungo kilichopandwa.


Viungo pia vinaweza kupandwa kwenye vyombo vya zamani ama vilivyovunjika


Baadhi ya viungo vilivyopandwa ndani ya nyumba na ni muhimu vikae karibu na dirisha ili vipate meanga wa kutosha


Jinsi ya kuweza kukuza viungo mimea (Herbs) ndani ya nyumba yako


Wakati mwingine ni garama sana kununua viungo sokoni na hii huwa changamoto kwa watu wengi sana. Hii inapelekea baadhi ya watu kuamua kutokutumia viungo kabisaa kwani wakijaribu kufananisha bei na kiasi anachopatiwa ni vitu visivyo endana. Hii ni kutokana na ukubwa wa bei wa viungo na umuhimu wa viungo katika mwili wa mwanadamu.
Kukuza ama kupanda viungo hivi ndani ya nyumba yako ama kukuzia nyumbani ndilo suluhisho pekee la kupunguza makali ya garama za kununua viungo. Garama hizi zinaweza kuzuilika tu pale utakapokuwa tayari kutumia sehemu kidogo ya jiko lako kukuza baadhi ya mimea ya viungo unavyovipenda sana. Haijalishi kama una uzoefu wa mimea ama hauna kwani ukuzaji huu wa mimea ni mrahisi sana. Ni ukuzaji mrahisi na hauitaji utaalamu wa hali ya juu katika ukulima huu. Kupanda na kukuza viungo ndani ya nyumba yako kuna garama nafuu kulinganisha na kununua viungo sokoni kunako ongeza garama kubwa ya maisha.
 
Oregano, Chives, mint, rosemary na Thyme ni viungo tunavyotumia sana kwenye chakula na ni rahisi kupanda na kukuza ndani ya nyumba yako. Kama ni mtu unaependa kupika sana, lazima utakuwa ni mpenzi wa viungo hivi mikononi mwako. Jifunze kutumia viungo hivi kwa garama nafuu ya kukuza ndani ya nyumba yako. Viungo hivi vinatumika sana kwenye mapishi ya nyama, mboga za majani, pilau, kachumbari, samaki, tambi na mengineyo.
Ili kukuza viungo hivi ndani ya nyumba yako ni muhimu kuweka karibu na sehemu zinazo ingiza mwanga kama dirishani, kwenye veranda ama karibu na milango. Mimea hii inahitaji mwanga wa kutosha hivyo ni muhimu kuhakikisha nyumba yako ina mwanga wa kutosha. Ni muhimu kukuza viungo hivi ndani kwani kuku na ndege wa aina mbali mbali upendelea kula mimea hii hivyo ni vizuri kukuza mimea hii ndani.
Unaweza kuamua kusia mbegu ili kuamisha baadae ama kununua miche ambayo tayari ilishaoteshwa mahali pengine na kuendeleza kilimo chako. Kuna baadhi ya container umbazo ni maalum kwa kukuzia mimea lakini pia inaweza kutumia vyombo vilivyo kwisha wakati wake ama (chipped) ama makontena ambayo yalishatumika kama madumu ya maji, mafuta ama ndoo za maji. Hakikisha vyombo hivi vina nafasi ya kutoa maji mara baada ya kumwagia mimea maji. Ni muhimu kuweka sahani ama kisosa chini ya chombo ili kuepusha maji kusambaa hovyo. Hakikisha kontena unalotumia lina nafasi ya kutosha ili kuwezesha mizizi kusambaa vizuri kuanzia inchi 6 hadi 12 kwenda chini. Unaweza kupanda mimea zaidi ya mmoja katika kontena moja. Hakikisha unaweka mbolea ya kutosha isizidi wala kupungua. Hakikisha mimea yako inapata maji ya kiasi, yasizidi wala kupungua sana. Ni vizuri kuhakikisha kila kontena unaweka label ya mmea uliopanda ili kuhakikisha unafuatilia ukuaji kwa karibu sana. Mara inapoona mimea yako imechepua na kuanza kutoa matoleo unaweza kuanza kutumia viungo vyako kwenye chakula. 
Kama unapenda kujaribu kupunguza matumizi ya kununua mimea iliyo tayari kukuza, ni vizuri kununua mbegu na kuanza kukuza mwenyewe lakini kumbuka hiyo itakuwa na kazi kubwa kwani utatakiwa kulea kama mtoto anavyo hitaji uangalizi wa karibui sana. Baada ya mbegu kuota utahitajika kuhamishia kwenye kontena utakalotumia kukuza mimea ya viungo.
Nakutakia ukuzaji mwema wa viungo ndani mwako na kwa wale watakao fanikiwa kukuza viungo ndani ya nyumba, mwaweza kunitumia picha Hapa na nitaziweka humu kwenye blog.

No comments:

Post a Comment