Maishafrika Adventure for the best Safari in East Africa

Wednesday, June 10, 2015

HARD WORKING WOMEN HOLIDAY

Watu wengi wamekuwa wakiniuliza unajuaje kwamba mtu ni hard working? ki ufupi tu mtu hard working ni yue anaefanya kazi kwa bidii zote na si lazima iwe kazi ya kuajiriwa tu hata kujiajiri mwenyewe ni part of it. Na kama ni mtu unaejiweza ni vizuri pia ukiwa kama muajiriwa wa mahala Fulani haitoshi hiyo peke yake bai ni vizuri kama unaweza kujiongeza. Nikisema kujiongeza namaanisha kuto kutegemea ajira tu bali kujaribu pia kuwa mjasiriamali pia hata kama ni kabiashara kadogo ni bora kuliko kutokuwa nayo kabisa. Pamoja na kuwa na yote hayo ni vizuri pia mwanamke chapakazi uwe ni mtu unaejua ku Save ama kwa Kiswahili sanifu uwe unajua kuweka akiba pia. Manake si kila siku ni siku ya asali, kuna kipindi mambo yanaweza kubadilika gafla na kama ni mtu wa kujiwekea akiba basi mambo yako yatakuendea poa na hakuna atakaejua mambo yako si poa. Kwahiyo basi mwanamkw unatakiwa kuwa chapakazi ama kitaalamu zaidi wanasema (Hard working woman), ujue kujiongeza, kujiwekea akiba, na pia usijibane sana ni lazima ujipe raha ama nene? Next time ntakuja na topic moja nzuri sana ya jinsi ya kuwa muajiriwa na mjasiria mali at the same time. SO MSIONE KAMA NAKULA BATA SANA, NAJUA PIA KUZITAFUTA NA NDO MAANA NAJUA KUZITUMIA PIA. See you next time.

 








No comments:

Post a Comment