I WISH YOU ALL EID MUBARAK
Monday, July 28, 2014
Saturday, July 26, 2014
MAMA MARIA
NYERERE
Viongozi
wametakiwa kuheshimu maoni ya wananchi wote bila kubagua ili kuepuka migogoro
isiyo ya lazima na kuendeleza Amani ya nchi iliyozoeleka.
Mke
wa Rais wa kwanza wa Tanzania Julias Nyerere, Maria Nyerere ametoa kauli hiyo
alipokuwa akizindua kitabu cha Dancing with destiny kilichotugwa na Urmila
Jhaveri
Mama
maria nyerere amesema hata kama mtu hajui kuandika wala kusoma mawazo yake
yanaweza kutumika na kuleta maendeleo nchini,
Mtunzi wa Kitabu hicho Urmila Jhaveri
amesema ametunga kitabu hicho kwa kuwa amezaliwa Tanzania na nia yake ni
kuonesha historia ya nchi enzi za mkoloni kitu ambacho kitachangia isipotee na
kusaidia vizazi vijavyo
Saturday, July 19, 2014
SERENGETI BOYS YAIKOSAKOSA AMAJIMBOS
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa
miaka 17, Serengeti Boys imelazimishwa sare ya bila kufungana na Afrika Kusini,
Amajimbos katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za Afrika, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanamaanisha, Serengeti Boys
itahitaji sare ya mabao katika mchezo wa ugenini, au kushinda kabisa ili
kuingia hatua ya mwisho ya mchujo katika kuwania tiketi ya Fainali zitakazopigwa
Niger mwakani.
Amajimbos waliuanza mchezo vizuri wakilitia
kwenye misukosuko lango la Serengeti kwa dakika takriban 20 za mwanzo, lakini
taratibu mchezo ulianza kubadilika na wenyeji wakageuza kibao.
Serengeti ilipoteza nafasi mbili za wazi za
kufunga kipindi cha kwanza na nafasi nyingine mbili zaidi za wazi pia za
kufunga kipindi cha pili, ambacho watoto wa nyumbani walitawala zaidi
mchezo.
Kocha wa Serengeti, Hababuu Ali alisema
kwamba vijana wake waliuanza mchezo kwa kuelemewa kutokana na woga wa kucheza
mbele ya umati wa mashabiki kwa mara ya kwanza lakini walipozoea waliendelea
vizuri.
Hababuu ameongeza kuwa Amajimbos si wazuri
kiufundi zaidi wana nguvu na kasi na kwa sababu hiyo ana matumaini ya kupata
matokeo mazuri ugenini.
Kikosi cha Serengeti Boys; Mitacha Mnacha,
Abdallah Jumanne/Mashaka Ngujiro dk23, Issa Baky, Adolph Mutasingwa/Kelvin
Farrel dk10, Martin Kiggi, Omar Wayne, Athanas Mdam, Ali Mabuyu, Abdul
Bitebo/Mohamed Mussa dk86, Prosper Mushi na Baraka Yussuf.
Amajimbos; Mondili Mpoto, Nelson Maluleke,
Simon Nqoi, Notha Ngcobo, Keanu Cupido, Tendo Mukumela, Katlego Mohamme,
Athenkosi Dlala, Sibongankonke Mbatha/Felix Noge, Luvuyo Mkatshana/Vuyo Mantjie
na Khanyiso Nayo.
Friday, July 18, 2014
HILI TUKIO LILITOKEA JANA HUKO MARANGU WILAYA YA MOSHI. HOUSE BOY ALIMKATA NA PANGA MTOTO WA MWENYE NYUMBA NA PANGA KICHWANI NA KUANZA KULA UBONGO WA MTOTO HUYO. HUYU MTOTO ALIKUWA YUPO DARASA LATATU NA ALISAHAU DAFTARI NYUMBANI. KURUDI TU ALIKUMBANA NA HOUAEBOY WAO NA KUYAFANYA HAYO. PICHA YA PILI NI YA HUYO HUSE BOY ALIEMUUA MTOTO. BAADA YA TUKIO HOUSEBOY ALIJIKATA SEHEMU ZAKE ZA SIRI MWENYEWE. INASEMEKANA KIJANA HUYU ALIRUKWA NA AKILI SIKU MOJA KABLA YA TUKIO NA HAKUNA ALIECHUKUA HATUA. MAJIRANI WANADAI WALIKUWA WANAFAHAMU KIJANA HUYO ALIKUWA NA KIFAFA SIKU ZA NYUMA. PICHA ZINATISHA TAFADHALI
Thursday, July 17, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)