Maishafrika Adventure for the best Safari in East Africa

Thursday, March 16, 2017

JINSI YA KUKUZA VIUNGO NDANI YA NYUMBA (Indoor Herb Garden)




Baadhi ya herbs unazoweza kupanda ndani ya nyumba yako


Baadhi ya Herbs zilizopandwa ndani ya nyumba kwa kutumia makopo ya plastic yaliyokwisha kutumika na kupakwa rangi monja

Upandaji wa Herbs kwa matumizi kama viungo na kutumika kama urembo wakati huo huo



Vikombe maalum vilivyotumika kupanda Herbs na kuandikwa aina ya herbs ili kufanya urahisi wa kutambua aina ya kiungo kilichopandwa.


Viungo pia vinaweza kupandwa kwenye vyombo vya zamani ama vilivyovunjika


Baadhi ya viungo vilivyopandwa ndani ya nyumba na ni muhimu vikae karibu na dirisha ili vipate meanga wa kutosha


Jinsi ya kuweza kukuza viungo mimea (Herbs) ndani ya nyumba yako


Wakati mwingine ni garama sana kununua viungo sokoni na hii huwa changamoto kwa watu wengi sana. Hii inapelekea baadhi ya watu kuamua kutokutumia viungo kabisaa kwani wakijaribu kufananisha bei na kiasi anachopatiwa ni vitu visivyo endana. Hii ni kutokana na ukubwa wa bei wa viungo na umuhimu wa viungo katika mwili wa mwanadamu.
Kukuza ama kupanda viungo hivi ndani ya nyumba yako ama kukuzia nyumbani ndilo suluhisho pekee la kupunguza makali ya garama za kununua viungo. Garama hizi zinaweza kuzuilika tu pale utakapokuwa tayari kutumia sehemu kidogo ya jiko lako kukuza baadhi ya mimea ya viungo unavyovipenda sana. Haijalishi kama una uzoefu wa mimea ama hauna kwani ukuzaji huu wa mimea ni mrahisi sana. Ni ukuzaji mrahisi na hauitaji utaalamu wa hali ya juu katika ukulima huu. Kupanda na kukuza viungo ndani ya nyumba yako kuna garama nafuu kulinganisha na kununua viungo sokoni kunako ongeza garama kubwa ya maisha.
 
Oregano, Chives, mint, rosemary na Thyme ni viungo tunavyotumia sana kwenye chakula na ni rahisi kupanda na kukuza ndani ya nyumba yako. Kama ni mtu unaependa kupika sana, lazima utakuwa ni mpenzi wa viungo hivi mikononi mwako. Jifunze kutumia viungo hivi kwa garama nafuu ya kukuza ndani ya nyumba yako. Viungo hivi vinatumika sana kwenye mapishi ya nyama, mboga za majani, pilau, kachumbari, samaki, tambi na mengineyo.
Ili kukuza viungo hivi ndani ya nyumba yako ni muhimu kuweka karibu na sehemu zinazo ingiza mwanga kama dirishani, kwenye veranda ama karibu na milango. Mimea hii inahitaji mwanga wa kutosha hivyo ni muhimu kuhakikisha nyumba yako ina mwanga wa kutosha. Ni muhimu kukuza viungo hivi ndani kwani kuku na ndege wa aina mbali mbali upendelea kula mimea hii hivyo ni vizuri kukuza mimea hii ndani.
Unaweza kuamua kusia mbegu ili kuamisha baadae ama kununua miche ambayo tayari ilishaoteshwa mahali pengine na kuendeleza kilimo chako. Kuna baadhi ya container umbazo ni maalum kwa kukuzia mimea lakini pia inaweza kutumia vyombo vilivyo kwisha wakati wake ama (chipped) ama makontena ambayo yalishatumika kama madumu ya maji, mafuta ama ndoo za maji. Hakikisha vyombo hivi vina nafasi ya kutoa maji mara baada ya kumwagia mimea maji. Ni muhimu kuweka sahani ama kisosa chini ya chombo ili kuepusha maji kusambaa hovyo. Hakikisha kontena unalotumia lina nafasi ya kutosha ili kuwezesha mizizi kusambaa vizuri kuanzia inchi 6 hadi 12 kwenda chini. Unaweza kupanda mimea zaidi ya mmoja katika kontena moja. Hakikisha unaweka mbolea ya kutosha isizidi wala kupungua. Hakikisha mimea yako inapata maji ya kiasi, yasizidi wala kupungua sana. Ni vizuri kuhakikisha kila kontena unaweka label ya mmea uliopanda ili kuhakikisha unafuatilia ukuaji kwa karibu sana. Mara inapoona mimea yako imechepua na kuanza kutoa matoleo unaweza kuanza kutumia viungo vyako kwenye chakula. 
Kama unapenda kujaribu kupunguza matumizi ya kununua mimea iliyo tayari kukuza, ni vizuri kununua mbegu na kuanza kukuza mwenyewe lakini kumbuka hiyo itakuwa na kazi kubwa kwani utatakiwa kulea kama mtoto anavyo hitaji uangalizi wa karibui sana. Baada ya mbegu kuota utahitajika kuhamishia kwenye kontena utakalotumia kukuza mimea ya viungo.
Nakutakia ukuzaji mwema wa viungo ndani mwako na kwa wale watakao fanikiwa kukuza viungo ndani ya nyumba, mwaweza kunitumia picha Hapa na nitaziweka humu kwenye blog.

Thursday, December 8, 2016

MATUMIZI YA VIKOMBE AMA GLASI ZILIZO VUNJIKA (CHIPPED)

Glass ama vikombe vilivyo vunjika ama (chipped)? Usivitupe vina kazi nzuri sana, fuatana name hapa kwenye blogu hii nikufahamishe.
 
Nilikuwa nikikasirika sana ninapoona glasi na vikombe vyangu nilivyokuwa navipenda nikivivunja ama kumeguka mara kwa mara na nilishindwa kuvitumia tena japo nilikuwa nikivipenda sana. Jambo hili limekuwa likinisumbua sana hasa kipindi cha miezi ya karibuni kwani nilijikuta nikivunja vyombo karibu kila siku. Nimejikuta kwa mwezi najaza ndoo ya takataka vyombo vilivyovunjika. Ndipo nilipotafuta njia ya kutumia vikombe ama glasi zangu zilizomeguka tena kwasababu nilikuwa nazipenda sana na ilikuwa ngumu kuzitupa kwani nilijua sitaziona tena. Hiki ndicho kilichao nifanya nitumie glasi hizo na vikombe kupanda maua ama kupanda viungo vya chakula.
 
Hakikisha unakusanya vikombe na glasi zilizomeguka, Tafuta maua madogo yasiyokuwa na mizizi mikubwa ama kuhitajo nafasi kubwa kukua. Jaza udongo wenye mbole  kwenye vikombe ama glasi na hakikisha unaweka mawe modogomadogo juu ya udingo ili ikusaidie kunyonya maji kwenye udongo kwani ukumbuke glasi ama kikombe hakina nafasi ya kupitisha maji kwa chini.
 
Mbanda mbegu zako ama panda miche ya maua ama viungo vya chakula. Kwangu mimi nilipanda maua yasiyo na mizizi mikubwa na nilipanda pia viungo kama giligilani, lettuce na green onions. Kwa kufanya hivi ilinipunguzia garama ya kununua giligilani na green onions kwakuwa nimekuwa nikizipata nyumbani kwangu baada ya kupanda kwenye kikombe. Na kwa wakati huo huo nyumba yangu una kuonekano mzuri sana kwakuwa kuna maua mazuri kwa muonekano tofauti.
 
Na pia nimekuwa nikiridhika pale ninapokiona kikombe change nilichokuwa nikikipenda ninakitumia tena kwa kuremba nyumba yangu. Tunatakiwa kutengeneza mazingira kwa kuepuka kutupa taka ngumu hovyo na kuhakikisha tunatafuta matumizi ya vyombo vilivyovunjika ambayo yatakuwa na faida wakati huohuo. Vikombe ama glasi hizi unaweza kupiga rangi ama kuremba kwa kuweka  ribbon ili kuwa na muonekano mzuri ila kama ni mtu wa kupenda kuchagua vyombo vizuri basi muonekano tu wa kikombe ama glasi yako unatosha.
 
 


Hii ni desert au ice cream glass iliyomeguka ambayo imetumika kupanda ua zuri. Na glasi hii unaweza kuiweka ndani ama barazani na ikapendezesha nyumba.



Hii ni glass ya maji iliyopata mpasuko (crake) ambayo imetumika pia kupanda uwa na linaweza kukaamahali popote kama urembo.
 
 


Hizi ni aina tofauti za vikombe vilivyomeguka na visosa vyake vilivyotumika kupanda mauwa na vimpendeza sana na kuvutia



 
Hizi ni glazi za maji za ukubwa tofauti zilizotumika kupanda mauwa ya aina moja, japo unaweza pia kupanda mauwa ya aina tofauti.




Hii pia ni glasi iliyotumika kupanda maua ya aina tofauti ila ni mauwa yenye mizizi midogo na haiitaji nafasi kubwa.

 
 
Hizi ni birika za chai ama maziwa zilizotumika kupanda maua ya aina tofauti na pia mauwa kama haya yanaweza pia kupambwa kwenye meza ya sebuleni (coffee table) ama meza ya chakula (dining table)
 
 
 


Hiki ni kikombe cha kahawa kilichotumika kupanda viungo vya kupikia na hii unaweza kuviweka pia jikoni mwako kwani vinahitaji mwanga mdogo.
 
 


 
hii ni chupa ya asali iliyokwisha kutumika ambayo imetumika kupansa uwa dogo. Na kwa kuremba chupa kama hii ambayo ina muonekano kabisa wa chupa unaweza kufunga kamba ya riboni ama kamba ya gunia safi na ikaonekana kuwa tofauti na kamba zingine.


 
Hiki ni kikombe cha chai kilichotumika kupanda uwa aina ya aloe vera ndogo na kama inavyookekana imekuwa na muonekano mzuri sana.
 
 

 
Haya ni matayarisho ya vikombe vilivyomeguka nikivitayarisha kwa kupanda viungo vya chakula.
 



 
Hizi ni glasi za mvinyo za aina tofauti nilizozitumia kupanda maua madogo na kuweka mawe madogi kwa juu.
 


 
 
Hivi ni vikombe vya chai vilivyotumika kupanda maua vikiwa katika muonekano mzuri.
 


Wednesday, November 23, 2016

MATUMIZI YA CHUPA ZA MVINYO ZILIZOKWISHA TUMIKA

Tumekuwa na mazoea ya kutupa chupa za mvinyo (wine) kila baada ya matumizi ya kinywaji hiki. Chupa hizi zinaweza kuwa na faida kubwa na pia kuwa na matumizi mbalimbali. Ni muhimu kuhifadhi mazingira kwa kujaribu kubadilisha matumizi ya chupa za mvinyo kwa kuzifanyia kazi tofauti kama kuremba na kupendezesha nyumba na maeneo tunayoishi.

unaweza kubadilisha matumizi ya chupa za mvinyo kama chungu cha kurembea maua (Flower verse) ama unaweza pia kutengeneza urembo mwingine wa kupendezesha nyumba yako. Unaweza kuchukua chupa ya wine iliyokwisha kutumika, ukaisafisha vizuri na kuipaka rangi unayopenda na hatimaye ikawa flower verse nzuri itakayopendezesha nyumba yako. Chupa hizi una uwezo wa kuiweka ndani ama nje ya nyumba yako.

Ni vizuri tuwe tunajaribu kutumia fursa kila tunapozipata, kwani hii si fursa ya kuremba nyumba tu ila inaweza kutumika kukuingizia kipato. Hii itakusaidia kuwa mjuzi zaidi na kujaribu kujifunza jinsi ya kuweza kutengeneza chupa hizi kwa ustadi zaidi.

Tunatakiwa kila wakati tuwe tunatafuta mawazo na uvumbuzi mpya, mawazo mapya, na kufikiri zaidi. Lakini kufikiria zaidi sio kufanya ama kutengeneza mambo mapya bali ni kujaribu kuishi kwa kuboresha mazingira kwa kubadilisha matumizi ya vitu ama bidhaa zilizokwisha kutumika ili kuweka mazingira safi kwa kuhakikisha bidhaa hizi zinatumika tena kama mpya. Tukiangalia sana kwenye mapambo ya nyumba utumiaji wa vitu vilivyotumika ni wa muhimu sana.
Na hii imesaidia badala ya kutupa chupa za mvinyo zilizokwisha kutumika tunazitumia kama mapambo ya nyumba. Chupa za wine zinaweza kudizainiwa na kubadilisha matumizi kwa kuzifanya kuwa urembo mahiri na tofauti nyumbani kwako. Chupa za mvinyo zinaweza kutumika kama flower verse, chungu cha maua na aina nyingine ya mapambo yanayoweza kufanya nyumba yako iwe na muonekano tofauti.

Kwa picha zilizopo hapa ninakuonyesha matumizi tofauti ya chupa za mvinyo zilizokwisha kutumika na jinsi gani unaweza kuzibadilisha na kuwa urembo nyumbani kwako. Njia zote za kuzipamba chupa hizi ni rahisi na pia hazina garama kubwa.

utahitaji baadhi ya vifaa katika urembaji wa chupa hizi, kama rangi za kusprey na si rangi za kupaka kwa mkono, gundi, kamba, inborn, na vifaa vingine kama mkasi n.k. hakikisha unasiku nzima ya kutosha na pia vifaa vingine unavyoviitaji utavijua pindi utakapokuwa tayari kwa kazi hii. Furahia kushinda ukiwa unafanya kazi na chupa za wine zilizokwisha kutumika.





Chupa hizi ni chupa za wine zilizokwisha kutumika, zikasafishwa vizuri na kutolewa lebo na kasha kupuliziwa rangi ya dhahabu ya kawaida, na hatimae zikapakwa urembo wa dhahabu katikati na chupa nyingine kupakwa juu. Zoezi hili ni rahisi na linachukua chini ya masaa mawili.Chupa hii inaweza kutumika kama flower verse nyumbani kwako ama kwenye sherehe yoyote. Zina muonekano wa kupendeza na kuvutia sana.




Unaweza pia kupuliza rangi ya silver kwenye chupa zako na rangi hiyo iwe ni rangi nyororo na pindi itakapokuwa imekauka vizuri paka kwa mkono rangi ya urembo wa silver ili chupa zako ziwe na muonekano mzuri. Epuka kupaka rangi tofauti ya urembo kwani chupa yako haitakuwa na muonekano mzuri. Chupa hizi unaweza kutumia kama flower verse ama kuzitumia kama urembo ndani ya nyumba yako.



Unaweza pia kupaka kila chupa na rangi tofauti, chupa hizi zilipakwa rangi ya kupuliza kwanza na hatimaye ilipakwa rangi ya urembo kwa juu ili kufanya rangi ya urembo kuwa imara zaidi na yenye muonekano wa kuvutia.



Hizi ni chupa za wine tofauti kwa ukubwa na upana, hapa ilitumika gundi na kamba nyembamba za rangi tofauti. Chupa hizi zilipakwa gundi ya maji (super glue haifai) na kuzungushwa kamba kwa ustadi mkubwa. Subiri hadi chupa ikauke vizuri na zitakuwa urombo mzuri wa ndani utakaopendezesha nyumba yako. Unaweza pia kubandika vifungo vya nguo za zamani ili kuongeza nakshi za chupa yako ama kuongezea kwa kutengeneza maua madogo ya nguo za zamani na kubandika na gundi juu ya kamba nyembamba juu ya chupa yako.



Watu wengi wamekuwa wakitumia mishumaa na kuweka ama kwenye kisosa au kununua mbao za kuweka mishumaa pale inapotumika ambapo huwa ni garama kubwa sana. Chupa za wine za ukubwa mbali mbali zinaweza kutumika ila hakikisha ni chupa iliyo na rangi moja na hakikisha unatoa lebo za kila chupa na chupa ibaki kama inavyoonekana kwenye picha. Utumiaji wa chupa hizi kwa matumizi ya mishumaa inafaa pale unapohitaji kutumia mishumaa mingi na si michache. Hii inaababisha mwanga wa mishumaa kufanya chupa zionekani na rangi tofauti na za kuvutia hasa nyakati za usiku.



Chupa za mvinyo zilizokwisha kutumika zinaweza pia kutumika katika bustani yako ya maua. Hii inasaidia bustani yako kuwa tofauti na ya kuvutia. Hii inapunguza matumizi ya mawe ama cement kuweka kingo za bustani yako ya maua. Huku ni kulinda mazingira na pia kupendezesha nyumba yako.

Chupa hizi za wine zinaweza pia kutumika kama flower verse kwenye garden yako na kwa garama nafuu tu. Chupa hizi kwenye picha zimesafisha ka kufungwa ama kuzungushiwa kitambaa nadhifu na kuwekwa maua na zinaonekana kuwa na muonekano mzuri sana. Unaweza kubadiliha aina ya vitambaa kutokana na zile rangi unazozipenda.


Kuremba na kupendezesha nyumba yako ni swala la muhimu na lakuvutia na haswa pale unapolinda mazingira. Natumai umejifunza kitu na kama utakuwa na swali ama wazo dondosha comment yako hapo na nitakujibu kwa muda muafaka.


Wednesday, September 21, 2016

JINSI UNAVYOWEZA KUTUMIA CHUPA YA PLASTIC KWENYE ENEO LAKO DOGO NA KUKUPA MANUFAA

Kuishi mijini kuna mazuri na changamoto zake, Uzuri kwamba kuna maisha mazuri na kujifunza mambo mengi zaidi kutokana na maendeleo ya eneo unaloishi. Pamoja na uzuri huo pia kuna changamoto zake ikiwemo ugumu wa maisha. Vijijini kuna changamoto ya ugumu wa maisha lakini mjini changamoto hii ni kubwa zaidi. Katika changamoto za kuishi mjini ni pamoja na garama za juu za chakula. malazi pamoja na mavazi. Na kutokana na ugumu wa maisha na garama za juu za chakula, mavazi na malazi mijini kunafanya watu kufunguka akili na kujua jinsi ya kupambana na changamoto hizi. Na kihi ndicho kilichonifanya mimi kuwaza sana na kufikiri hili jambo ninalotaka kulielezea hapa.
 
leo hii nimegundua kwamba tuna njia nyingi sana za kupambana na ugumu wa maisha. Katika maisha ya kila siku tunatumia garama nyingi sana kwenye chakula na malazi. Na kwa sababu hiyo inatulazimu kutafuta ama kuishi katika nyumba zenye maeneo madogo na hayana nafasi maalum ya kuzalisha chakula kitakacoweza kukimu mahitaji ya familia. Lakini hii tusiione kama changamoto kwani kuna njia nyingi sana ya kuzalisha vyakula vya kukimu familia zetu hata kwa yale maeneo madogo tunayoishi. Hii ni kwa kutumia makopo ama chupa za plastic kwa kukuza mboga za majani katika uwa mdogo wa nyumba yako.
 
Nafasi ndogo nyumbani kwako isiwe sababu ya wewe kutumia garama kubwa kununua mboga na viungo vya chakula nyumbani kwako. Kwa nafasi ndogo uliyonayo una uwezo wa kuhakikisha unapunguza garama za maisha za kununua chakula. Hii ni kwa kuhakikisha unatafuta makopo ama chupa za plastiki zilizokwisha kutumika kama nilivyoonyesha kwenye picha hizi. tafuta udongo mzuri na kama utapata mbolea ya kuku itakuwa ni vizuri zaidi. Hii ni kwasababu mbolea ya kuku haina takataka zinazoweza kusababisha kuota magugu ama majani yasiyohitajika kwenye makopo yako. Unaweza pia kutumia mbolea ya ng'ombe ila uwe tayari kung'oa magugu kwenye chupa zako kila wakati. Hii ni kwasababu Ng'ombe hula majani na matunda ya aina mbalimbali na kuyatoa kwenye kinyesi yakiwa hai ama kuwa na uwezo wa kuota tena. Unaweza kuchanganya udongo wako na mbolea ya kuku pembeni ka kuuacha kwa wiki moja ili ujichanganye vizuri na kasha kuujaza kwenye makopo yako tayari kwa kusia mbegu ama kupanda miche ya mboga na matunda unayoyahitaji katika uwa mdogo wa nyumba yako.
 
 
Siwezi kuacha kusema kwamba uzalishaji huu una manufaa makubwa na msaada mkubwa kwa familia. Uzalishaji huu wa mboga za majani utapunguza garama kubwa za maisha yako na pia familia yako itajipatia lishe bora. Zoezi hili ni zuri kwa sababu unalinda mazingira kwa kuhakikisha makopo ya plastic yanahifadhiwa vizuri na kuzalisha chakula kwa familia, kwani kwa kutumia makopo mia ya plastiki una uwezo wa kilisha familia yako mwaka mzima chakula bora kwa garama kidogo. Hii inawezekana kwa kutengeneza frame ndogo kwenye uwa wako na kutengeneza nafasi ya kuhifadhi maji utakayoyatumia kumwagia mimea yako kuifadhiwa na kutumika baadae. Uzalishaji huu wa mboga za majani unahifadhi si eneo tu bali unahifadhi pia maji kutopotea ardhini bali kubaki katika eneo ulilotenga chini ya fremu yako ya mbao na kutumia tena kumwagilia mimea siku inayofuata. Kiufupi ukulima huu unatumia nafasi ndogo, garama kidogo, kuhifadhi maji na kuipa familia yakko chakula bora na afya bora. Mimi nimechukua hatua kwa kufanya hivi nyumbani kwangu, na wewe chukua hatua na utaona umuhimu wa hili ili kupunguza njaa majumbani mwetu.
 
 
 
Chupa za soda kubwa zilizotumika kuotesha vitunguu 
 
 
Mboga aina ya lettuce iliyooteshwa kwenye makopo ya juice na mafuta yaliyokwishatumika

 
 

Frame ya mbao iliyopangiliwa chupa za juice na mafuta kwa ustadi mkubwa zilizo oteshewa nyanya, Vitunguu, lettuce na mboga zingine. Kwa chini inaonekana kabwawa kadogo kanachohifadhi maji yanayotoka kwenye makontena baada ya kunyeshea. Huu ni uhifadhi mkubwa wa maji na ukulima huu unafaa hata sehemu zenye shida ya maji.


Ni nani asiependa kuwa na kontena zilizosheheni mboga za majani, matunda na viungo kwenye uwa mdogo wa nyumba yako? Ni kwa kutumia chupa na madumu ya plastiki yaliyokwisha kutumika yanaweza kufanya haya. Unasafusha mazingira kwa kuwekeza kwenye chakula cha familia yako kwa garama nafuu. 


Chupa na makopo yaliyotumika yakiwa katika fremu ya mbao ama miti.


Fremu ya mbao ya bei rahisi unayoweza kutumia kupanga makopo yako ya kuoteshea mboga. Ujanzi huu ni wa garama rahisi sana usiozidi shilingi 50,000 za kitanzania. Unachukua sehemu ndogo na unahifadhi maji kama inavyoonekana chini ya fremu hii, unapomwagia maji mboga zako hayapotei bali kuingia moja kwa moja kwenye bwawa dogo chini ya makopo na unaweza kutumia maji hayo kunyeshea mboga zako siku inayofuata. Fremu hii ina uwezo wa kubeba makopo mia moja inategemea na ukubwa utakaoutaka.



Upandaji huu wa mboga utakusaidia kuboresha afya ya kwako na familia yako kwa garama ndogo.


 
 

Thursday, March 24, 2016

AINA YA WATU UNAOWEZA KUKUTANA NAO KATIKA MAISHA YA KILA SIKU

 
 
 



Katika maisha ya kila siku utakutana na watu wa aina tofauti, ni jambo la muhimu sana kujifunza jinsi ya kuishi na watu wa aina hii. Unatakiwa kuwa mtulivu na kuhakikisha unampuuza na kufanya mambo ya muhimi na kuepuka watu wa namna hii
Naamini utakuwa tayari umekutana na watu wa aina tofauti na wenye tabia tofauti, inaweza kuwa kwenye maeneo ya kazi, labda ni marafiki zetu, na pengine tunaishi nao ama ni wanafamilia wetu. Jambo la muhimu ni kukwepa hawa watu, na kuwakwepa mapema zaidi ni jambo la busara. Posti hii itaongelea aina ya watu wa namna hii na jinsi ya kuwakwepa.

Watu wanaopenda sana Kuhukumu
Watu wa namna hii hupenda kuhukumu kila kinachotokea ama kusikia mbele yao. Unaweza ukawa unajaribu kuzungumza nae ama kumuelekeza lakini atahukumu (judge) kila moja kati ya yale uliyomweleza ama kuona. Hupenda kumaliza mazungumzo kwa kuhukumu bila kutaka kujua lengo hasa la kumweleza na ni wagumu sana kuwasiliana. Utakapotaka kutoa ushauri ama kupata ushauri kutoka kwa watu wa namna hii ni kupoteza muda. Kwasababu atahukumu kile anachokijua badala ya kukupa maelezo ama kutoa ushauri.

Watu wenye wivu
Kuna watu wenye wivu, wapo kila mahali. Watu wa namna hii ni wale ambao hawafurahi wanapokuona una mafanikio na kujaribu kugeuza yale mazuri na kuwa mabaya. Jaribu kuepuka watu wa namna hii kwasababu watashirikiana na maadui zako kukuangamiza ama kurudisha nyuma mafanikio yako. Wanahisi kwamba mambo mazuri yanatakiwa kutokea kwao tu na si kwa mtu mwingine.

Wale wajuaji kupindukia
Watu hawa huwa si wasikivu, na hawako tayari kusikiliza mtu, kwasababu kutokana na ujuaji wao wanaona kama hakuna anaejua bali wao tu ndiyo wanaojua kila kitu. watu kama hawa wanaweza kuwa kidonda katika maisha yako binafsi, ni watu wasiofaa kuwa nao karibu katika maisha yako ya kila siku. Ukitaka kuwa na mafanikio katika maisha yako hakikisha unakaa mbali na watu kama hawa.

Watu wajinga (arrogant)
Usije ukafananisha kujiamini na ujinga, watu wanaojiamini ni watu ambao kila mtu anatamani kuwa nao wakati wote, wakati watu wajinga wanakasirisha na kuchukiza kabisa. Mtu mwenye tabia za kijinga hujisikia yeye ni bora zaidi ya mwingine. Jaribu kuepuka kabisa watu wa namna hii kwasababu itakuepushia mazingira ya yeye kukukwaza kutokana na ujinga wake.

Watu wanao laumu
watu wanaolaumu kawaida wanapokosea hupenda kulaumu watu kwa makosa waliyoyafanya na si kukubali kwamba wamekosea. Ni watu ambao wapo na tunaishi nao katika mazingira ya kila siku. Watu hawa hawawezi kupewa majukumu na wakayabeba yale majukumu, na wakati wote hupenda kunyooshea watu vidole na hii uathiri sana yale majukumu waliyopewa kuyasimamia. Jaribu kuwaepuka sana watu hawa.

Wale wanaokuwa na maono hasi
watu wa namna hii ni watu wanaoweza kukukatisha tamaa mapema sana. Hawezi kukupa mawazo ambayo yatakupa moyo na kukupa nguvu ya kufanya kitu Fulani. Bali watakukosoa kwa kila utakalojaribu kuwaambia au kufanya na watahakikisha wanafanya vyovyote vile unalojaribu kufanya lisifanikiwe.

Watu waongo.
unapotaka kufanikiwa lazima uzungukwe ama ukutane na watu ambao nao pia wana mafanikio na ambao utawaamini wao kukufikisha pale unapotaka. Unapokutana na nmtu kama huyu uwezi kuamini na ni ngumu kuwategemea kwasababu hujui kama wanakwambia ukweli ama uongo. Epuka watu waongo na kaa nao mbali kwasababu hutafahamu wakati gani watakudanganya ama kukueleza ukweli.

Watu wambea (wadaku)
Watu huwa wambea kwasababu hawajiamini na hawajui jinsi ya kutenganisha mambo ya ukweli na uongo na badala yake huyasuka na matokeo yake ni kuwa uongo. Wtu hawa uchukua taarifa za uongo na kuzivisha ukweli na mwisho wa siku zinakuja kusababisha uadui usiokuwa na tija ama kusababisha madhara kabisa. Kuwa na mtu mmbea kwenye maisha yako inaweza kukuaribia maisha yako na ni kama ugonjwa wa saratani na unaweza kukuletea madhara katika maisha yako ya kila siku.

Kama katika hizi kengele 8 kuna kengele moja wapo ama zaidi inalia katika maisha yako inawezekana ukashindwa kupata mafanikio katika haya maisha ya sasa. Unachotakiwa ni kuhakikisha una epukana na watu wa namna hii mapema iwezekanavyo. Jaribu kuwa na ukaribu na watu ambao ni chachu kwenye mafanikio yako. Mimi nimeamua kuepukana na aina hizi nane za watu niliowaongelea hapo juu mwaka huu 2016 na kwa kufanya hivi nimejijengea mazingira mazuri katika maisha yangu na kwa mungu pia.


Monday, March 21, 2016

HOW TO BE STRONG INDEPENDENT WOMAN



Being a strong, independent woman inamaaisha una uwezo wa kujiamini  na kuishi maisha yako.Unatakiwa kujiamini bila kutegemea mtu yeyote ama jamii yako kukufanya ujiamini. Namaanisha uwe na uhuru wa fikira na kuwa na afya na mahusiano na watu wengine. Namaanisha jifunze jinsi ya kujitambua wewe ni nani, hata kama una aibu  na kuzungumza polepole ama kwa sauti kubwa. Nifuatilie katika posti hii ili utambue ni jinsi gani unaweza kuwa mwanamke anaejiamini na unataka kuwa nani.

Jifikirie wewe kwanza
Utakapojitambua wewe mwenyewe, utajua ni kitu gani unahitaji maishani mwako. Kama unataka watu kujua unachokifanya jitayarishe kuweka mazingira hayo. Fanya kile moyo wako unapenda ili mradi kiwe ni sahihi na kina manufaa kwako. Siku zote sikiliza kile moyo wako unakwambia na kile ambacho ukikifanya unasikia amanai. Pale utakapokuwa tayari kutimiza yale yanayokufuraisha itakusaidia kujenga mahusiano mazuri na watu wa karibu yako. Hii itakusaidia mahusiano yako yawe boara kwasababu wewe mwenyewe unajitambua na itasaidia kumweleza mpendwa ama mpenzi wako wewe ni nani na unataka nini.

Jifunze jinsi ya kutambua mawazo yako
Ukijifunza jinsi ya kujitambua utajua kwamba mahusiano yako yanatambulisha maisha yako halisi. Moja kwa moja utakuwa ni mtu wa kumfikiria mwenzano na kusubiri maamuzi baada ya kuwasiliana na mwenzako. Pambana ili ujitambue, na usitake matatizo yako kupambana nayo mwenyewe. Jaribu kuwasiliana na watu wako wa karibu ili wakusaidie katika ushauri.

Usijifananishe na wanawake wengine
Kuwa na mtu unaemuangalia na kutamani kuwa kama yeye ni swala zuri, Lakini unatakiwa kuwa mwangalifu na usiangukie kwenye wivu ama tamaa kwa mtu huyo unaetamani kuwa kama yeye (Role Model). Japo kuwa na wivu ni asili ya kila mwanadamu lakini jifunze jinsi ya kuzuia hilo kutokea. Jaribu kutambua kila unaposikia wivu, hatua ya kwanza unapojitambua umeona wivu jaribu kusahau mara moja. Huwezi kufanana na mtu yeyote. Wewe unaweza kujiona una mapungufu na pia watu wanaokutazama kuna wanaopenda kuwa kama wewe. Jaribu kujikumbusha kuwa kila mtu amepangiwa maisha tofauti na yako na labda huyo unaemuonea wivu anatamani kuwa kama wewe. Sio kila mwenye mafanikio ameyapata kwa urahisi, bali wamepitia ama kufanya mambo mabaya kupita kiasi.

Jaribu kuwa na mipaka
Jaribu kuhakikisha unakuwa na mipaka na kujali yale muhimu katika maisha yako. Weka mipaka na angalia muda unao spend na watu. Hakikisha una mambo mengine ya kufanya katika maisha yako nje ya mahusiano uliyokuwa nayo, kama ni shule, kazi, marafiki, kwenda kwenye mazoezi au familia yako. Kuwa na mipaka na kila mtu na wasiliana nao pale unapowaitaji na si kila wakati, hii itakusaidia kuwa na maisha yako binafsi.

Simama kwa miguu yako
Kama wewe ni mwanaume ama mwanamke, unatakiwa kujifunza kusimama kwa miguu yako, hii itakusaidia kwa watu wengine kutokuchukua nafasi ya matatizo yako kama mtaji. Jifunze jinsi ya kusema hapana. Jaribu kuishi maisha ya kujitegemea na si ya kutegemea kusaidiwa na watu. Tafuta kazi ama shuguli yoyote itakayokuingizia kipato. Unapokuwa na tatizo jaribu kutafakari suluhisho la tatizo lako na si kusubiri rafiki jamaa ama ndugu kukusaidia kuamua ama kuchukua hatua.

Jifunze kusema hapana
Jiweke wewe mbele kwanza badala ya kuweka watu wengine kwanza. Kwa mfano  mtu anakuomba umkopeshe pesa, si lazima umkubalie kila mtu. Hata kama rafiki yako atataka kukuazima gari mueleze gari halipo tena. Usijaribu kuwa mzuri kwa kila mtu. Jaribu kujifunza kusema hapana kwasababu kuna watu watatumia mwanya wa wewe kutokuwa na mamlaka na kilicho chako kwa manufaa yao binafsi.

Jiamini
Utakapojiamini kwamba unaweza na una ujaribu, utakuwa na ujasiri mkubwa sana. Timiza malengo yako na kile unachokitaka.  Unapokosa kujiamini ama unakaribia kuwa mtu wa namna hiyo, utafanya watu wakutumie kutimiza malengo yao badala ya wewe kutimiza malengo yako.

Fanya watu wako wa karibu wafahamu pale wanapokukera ama kukukwaza
Kama mtu amekukwaza kwa njia yoyote ile, hakikisha unamfahamisha. Wakati mwingine inakuwa vigumu kuonyesha unavyojisikia hasa unapokuwa na hasira.  Lakini kwa kumwambia mtu unavyojisikia itakusaidi kuzuia mtu kukukwaza ama kukukasirisha tena. Jaribu kuepuka kuzungumza na mtu pale unapokuwa na hasira kali. Kwani hiyo itapelekea kuzungumza maneno ambayo hayatatengeneza bali yataharibu. Kuwa na subira na zungumza na aliyekuwaza pale hasira yako itakapokuwa imetulia.

Thursday, February 18, 2016

SO YOU WANT TO BE YOUR OWN BOSS?

 

 
So You Want to Be Your Own Boss?
 
 

Kama unataka kuanza biashara na hujui pa kuanzia, usihofu, haupo peke yako. Watu wengi wanapenda kufanya kazi wanazo zipenda, na zile zitakazo wawezesha kutimiza malengo yao. Usijali lolote cha muhimu ni kuhakikisha unakuwa bosi wako mwenyewe, na hii unaweza kuanza leo hii unaposoma hii blog.
Yafuatayo ni mambo yanayoweza kukusaidia kutimiza malengo yako;
Jithaminishe uwezo wako na hakikisha unajiamini kuwa ni wewe tu utakae timiza lengo hili. Je unatakiwa kulaumu uchumi? muajiri wako, mpenzi wako ama familia yako?  Mabadiliko yanaweza kutokea tu kama utachukua maamuzi magumu.
Chagua biashara nzuri utakayo iweza. Jipe ruhusa ya kupambanua mambo. Kuwa huru kuangalia mambo tofauti yanayokuzunguka. Angalia muonekano wako, staili ya maisha ya jamii iliyokuzunguka na umri wa jamii inayokuzunguka. Mara nyingi hatukubaliani na hili lakini ni jambo muhimu sana katika kutimiza ndoto hii. Jiulize ni nini kitakupa nguvu hata pale utakapokuwa umechoka.
Kuna mambo matatu yatakusaidia kujua biashara unayoifanya ni sahihi.
Siku zote fanya biashara unayoijua, angalia muda uliokuwa ukifanya kazi kwa muajiri wako na fikiria utaalamu huo ukiufanya kwenye biashara yako itakuwaje.
Jaribu kufanya kile wengine wanachokifanya, jifunze kupitia biashara inayofanana na ya kwako. Na hapo utatambua kama ndiyo biashara unayoifahamu na usisite kuanza.Jaribu kutafuta suluhisho ya changamoto unayofikiria yanaweza kutokea katika biashara hiyo baada ya uchunguzi. Je kuna nafasi kwenye soko? Je huduma ama bidhaa unayotaka kutoa inahitajika katika soko sana? kama jibu ni ndiyo ingiza bidhaa hiyo ama huduma hiyo. Hakikisha unapochukua maamuzi unajitolea kujifunza na kupata uzoefu kabla ya kuanza kutumia mtaji wako.
Hakikisha unatengeneza mchanganuo wa biashara ili kukuwezesha kufanikiwa.
Watu wengi hawapendi kutengeneza mchanganuo wa biashara (Business plan), lakini itakusaidia kulifikia soko mapema. Mchanganuo wa biashara utakusaidia kuiweka sawa biashara yako, kujiamini na kufikia malengo. Mchanganuo wako hautakiwi kuzidi upande mmoja wa karatasi. Unatakiwa kuandika malengo, mategemeo na vitendo hatua kwa hatua, na biashara yako itakuwa kubwa.
Jiulize maswali yafuatayo:
Ninajenga nini?
nitamuhudumia nani?
Ninatoa ahadi gani kwa wateja wangu/na kwangu mimi mwenyewe?
Malengo yangu ni nini, mipangilio na hatua ntakazo piga kufikia malengo yangu?
Jua kundi unalolihitaji kufanya nao bishara kabla hujagarimia chochote

Kabla hujaanza kugarimia biashara, jaribu kafuatilia kama watu watakuwa tayari kununua bidhaa ama huduma unayotaka kuitoa. Hili ni jambo la muhimu sana kulifanyia kazi. Unaweza kulifanya hili kwa kulinganisha soko lako la biashara unayotaka kuifanya. Kwa maneno mengine ni nani haswa atanunua bidha au huduma yako zaidi ya familia na rafiki zako? ( Na usiseme kilamtu Tanzania hii anahitaji huduma unayoitoa, "Niamini hakuna kitu kama hicho") jaribu kufikiria ukubwa wa watu unao walenga? Wateja wako ni kina nani? Je bidhaa yako ama huduma yako ni ya muhimu sana katika maisha yao ya kila siku? na ni kwanini wanaihitaji?
Angalia kipato chako na chagua njia sahihi ya kupata fedha unazozihitaji katika biashara yako. Kama mjasiriamali, maisha yako binafsi yanachangia katika  hili. Una uwezo wa kuwa mmoja kati ya wawekezaji wakubwa. Hivyo unatakiwa kuwa na uelewa mkubwa wa kipato chako halisi, na uwezekano wa kutafuta kipato hicho, ni hatua muhimu ya kwanza kabla ya kutafuta mtaji nje wa biashara yako. Hili ni muhimu ndiyo sababu ya kusisitiza kwenye post zangu zilizopita kwamba tunatakiwa kujifunza kujiwekea akiba. Ukiwa unatengeneza mchanganuo wa biashara, unatakiwa kulipa uzito swala la mtaji kutokana na biashara unayotaka kuifanya, kutegemeana na eneo unalotaka kufanyia biashara. Ni muhimu kuhakikisha una mtaji wa kuanzisha biashara yako, na ni muhimu kufahamu aina ya fedha utakazokubali zitumike katika biashara yako ( kwa mfano kupokea fedha za nje, Credit Card, etc), ni lazima ukubaliane na haya katika kukuza biashara yako.
Jenga mtandao
Ukisha jenga malengo ya biashara yako, unahitajika kujenga mtandao wa watakao kuunga mkono, washauri, wawekezaji wenzako, watakao kupa huduma na watakao tembeza ama kuitangaza biashara yako. Kama utaiamini biashara yako na wengine wataiamini pia.
Jenga mitandao kitaifa na kimataifa, na kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram, Face book, Twitter, n.k na kwenye magroup mengine ya kibiashara.  

Uza bidhaa ama huduma yako kutokana na thamani yake. Hata kama tunanunua na kuuza bidhaa ama huduma kila siku,  watu hawataki kuuziwa vitu bei gali, jaribu kusaidia watu kwa kuuza bai stahili. Jinsi unavyotoa huduma kwa watu wengi, unaongeza mauzo na idadi ya kipato chako. kama ni mjasiriamali unaemjali mteja wako lazima utajiuliza maswali yafuatayo:
Je ninaweza kuwapa  nini?
Je nitafanyaje ili waridhike na huduma ama biashara ninayo ifanya kwao?
Haya maswali mawili yatakusaidia kukuongoza kwenye njia mpya katika bidhaa yako ama huduma yako na kuiongezea thamani, ambayo wateja wako wataridhika.
Kuwa tayari kusema wewe ni nani, na unafanya nini bila kuwa na uwoga. Hakikisha unafanya hivyo kwenye Mitandao ya kijamii, ili kujitangaza na kuitangazia dunia.
Jaribu kufanya kile unachodhani kitafurahisha followers wa biashara yako.

Pamoja na kwamba mitandao ya kijamii ina umuhimu kwa sasa ni muhimu kuitumia, na pia sisite kutumia njia nyingi za kutangaza biashara yako, kama kwenda kueleza watu wewe mwenyewe kuhusu bidhaa ama huduma unayoitoa, website, blog post, speech, news latter, simu n.k. Kama utafuata hatua hizo hapo juu, utakuwa vizuri na utakuwa njiani kuwa bosi wako wewe mwenyewe. ni muhimu kukumbuka haupo peke yako. Kama unataka kuwa bosi wako mwenyewe lakini unaona umekwama, jiunge na wajasiriamali wengine kwa nia tofauti. Utashangaa kupata habari za wajasiria mali walio fanikiwa wakieleza mapito yao magumu kufika hapo walipofika na itakuwa ni njia nzuri ya mawasiliano yatakayokuwa ni chachu katika biashara yako na utagundua mafanikio yako yapo katika  pingili za viganja vya mikono yako.
Ndoto yangu ya kuwa my own boss ni hiyo picha hapo juu, Ninafanya kazi kwa bidii sana kuhakikisha naitimiza, ninasali sana na ninaweka akiba ipasavyo kuhakikisha natimiza lengo langu hilo. "Lets work hard, lets save money, lets achieve our goals. Lets work hard and pay our bills". "My dream business in coming years" "Pergola .....!!!"