Maishafrika Adventure for the best Safari in East Africa

Thursday, March 24, 2016

AINA YA WATU UNAOWEZA KUKUTANA NAO KATIKA MAISHA YA KILA SIKU

 
 
 



Katika maisha ya kila siku utakutana na watu wa aina tofauti, ni jambo la muhimu sana kujifunza jinsi ya kuishi na watu wa aina hii. Unatakiwa kuwa mtulivu na kuhakikisha unampuuza na kufanya mambo ya muhimi na kuepuka watu wa namna hii
Naamini utakuwa tayari umekutana na watu wa aina tofauti na wenye tabia tofauti, inaweza kuwa kwenye maeneo ya kazi, labda ni marafiki zetu, na pengine tunaishi nao ama ni wanafamilia wetu. Jambo la muhimu ni kukwepa hawa watu, na kuwakwepa mapema zaidi ni jambo la busara. Posti hii itaongelea aina ya watu wa namna hii na jinsi ya kuwakwepa.

Watu wanaopenda sana Kuhukumu
Watu wa namna hii hupenda kuhukumu kila kinachotokea ama kusikia mbele yao. Unaweza ukawa unajaribu kuzungumza nae ama kumuelekeza lakini atahukumu (judge) kila moja kati ya yale uliyomweleza ama kuona. Hupenda kumaliza mazungumzo kwa kuhukumu bila kutaka kujua lengo hasa la kumweleza na ni wagumu sana kuwasiliana. Utakapotaka kutoa ushauri ama kupata ushauri kutoka kwa watu wa namna hii ni kupoteza muda. Kwasababu atahukumu kile anachokijua badala ya kukupa maelezo ama kutoa ushauri.

Watu wenye wivu
Kuna watu wenye wivu, wapo kila mahali. Watu wa namna hii ni wale ambao hawafurahi wanapokuona una mafanikio na kujaribu kugeuza yale mazuri na kuwa mabaya. Jaribu kuepuka watu wa namna hii kwasababu watashirikiana na maadui zako kukuangamiza ama kurudisha nyuma mafanikio yako. Wanahisi kwamba mambo mazuri yanatakiwa kutokea kwao tu na si kwa mtu mwingine.

Wale wajuaji kupindukia
Watu hawa huwa si wasikivu, na hawako tayari kusikiliza mtu, kwasababu kutokana na ujuaji wao wanaona kama hakuna anaejua bali wao tu ndiyo wanaojua kila kitu. watu kama hawa wanaweza kuwa kidonda katika maisha yako binafsi, ni watu wasiofaa kuwa nao karibu katika maisha yako ya kila siku. Ukitaka kuwa na mafanikio katika maisha yako hakikisha unakaa mbali na watu kama hawa.

Watu wajinga (arrogant)
Usije ukafananisha kujiamini na ujinga, watu wanaojiamini ni watu ambao kila mtu anatamani kuwa nao wakati wote, wakati watu wajinga wanakasirisha na kuchukiza kabisa. Mtu mwenye tabia za kijinga hujisikia yeye ni bora zaidi ya mwingine. Jaribu kuepuka kabisa watu wa namna hii kwasababu itakuepushia mazingira ya yeye kukukwaza kutokana na ujinga wake.

Watu wanao laumu
watu wanaolaumu kawaida wanapokosea hupenda kulaumu watu kwa makosa waliyoyafanya na si kukubali kwamba wamekosea. Ni watu ambao wapo na tunaishi nao katika mazingira ya kila siku. Watu hawa hawawezi kupewa majukumu na wakayabeba yale majukumu, na wakati wote hupenda kunyooshea watu vidole na hii uathiri sana yale majukumu waliyopewa kuyasimamia. Jaribu kuwaepuka sana watu hawa.

Wale wanaokuwa na maono hasi
watu wa namna hii ni watu wanaoweza kukukatisha tamaa mapema sana. Hawezi kukupa mawazo ambayo yatakupa moyo na kukupa nguvu ya kufanya kitu Fulani. Bali watakukosoa kwa kila utakalojaribu kuwaambia au kufanya na watahakikisha wanafanya vyovyote vile unalojaribu kufanya lisifanikiwe.

Watu waongo.
unapotaka kufanikiwa lazima uzungukwe ama ukutane na watu ambao nao pia wana mafanikio na ambao utawaamini wao kukufikisha pale unapotaka. Unapokutana na nmtu kama huyu uwezi kuamini na ni ngumu kuwategemea kwasababu hujui kama wanakwambia ukweli ama uongo. Epuka watu waongo na kaa nao mbali kwasababu hutafahamu wakati gani watakudanganya ama kukueleza ukweli.

Watu wambea (wadaku)
Watu huwa wambea kwasababu hawajiamini na hawajui jinsi ya kutenganisha mambo ya ukweli na uongo na badala yake huyasuka na matokeo yake ni kuwa uongo. Wtu hawa uchukua taarifa za uongo na kuzivisha ukweli na mwisho wa siku zinakuja kusababisha uadui usiokuwa na tija ama kusababisha madhara kabisa. Kuwa na mtu mmbea kwenye maisha yako inaweza kukuaribia maisha yako na ni kama ugonjwa wa saratani na unaweza kukuletea madhara katika maisha yako ya kila siku.

Kama katika hizi kengele 8 kuna kengele moja wapo ama zaidi inalia katika maisha yako inawezekana ukashindwa kupata mafanikio katika haya maisha ya sasa. Unachotakiwa ni kuhakikisha una epukana na watu wa namna hii mapema iwezekanavyo. Jaribu kuwa na ukaribu na watu ambao ni chachu kwenye mafanikio yako. Mimi nimeamua kuepukana na aina hizi nane za watu niliowaongelea hapo juu mwaka huu 2016 na kwa kufanya hivi nimejijengea mazingira mazuri katika maisha yangu na kwa mungu pia.


No comments:

Post a Comment