Thursday, March 24, 2016
Monday, March 21, 2016
HOW TO BE STRONG INDEPENDENT WOMAN
Being a strong, independent woman inamaaisha una uwezo wa kujiamini na kuishi maisha yako.Unatakiwa kujiamini bila kutegemea mtu yeyote ama jamii yako kukufanya ujiamini. Namaanisha uwe na uhuru wa fikira na kuwa na afya na mahusiano na watu wengine. Namaanisha jifunze jinsi ya kujitambua wewe ni nani, hata kama una aibu na kuzungumza polepole ama kwa sauti kubwa. Nifuatilie katika posti hii ili utambue ni jinsi gani unaweza kuwa mwanamke anaejiamini na unataka kuwa nani.
Jifikirie wewe kwanza
Utakapojitambua wewe mwenyewe, utajua ni kitu gani unahitaji maishani mwako. Kama unataka watu kujua unachokifanya jitayarishe kuweka mazingira hayo. Fanya kile moyo wako unapenda ili mradi kiwe ni sahihi na kina manufaa kwako. Siku zote sikiliza kile moyo wako unakwambia na kile ambacho ukikifanya unasikia amanai. Pale utakapokuwa tayari kutimiza yale yanayokufuraisha itakusaidia kujenga mahusiano mazuri na watu wa karibu yako. Hii itakusaidia mahusiano yako yawe boara kwasababu wewe mwenyewe unajitambua na itasaidia kumweleza mpendwa ama mpenzi wako wewe ni nani na unataka nini.
Jifunze jinsi ya kutambua mawazo yako
Ukijifunza jinsi ya kujitambua utajua kwamba mahusiano yako yanatambulisha maisha yako halisi. Moja kwa moja utakuwa ni mtu wa kumfikiria mwenzano na kusubiri maamuzi baada ya kuwasiliana na mwenzako. Pambana ili ujitambue, na usitake matatizo yako kupambana nayo mwenyewe. Jaribu kuwasiliana na watu wako wa karibu ili wakusaidie katika ushauri.
Usijifananishe na wanawake wengine
Kuwa na mtu unaemuangalia na kutamani kuwa kama yeye ni swala zuri, Lakini unatakiwa kuwa mwangalifu na usiangukie kwenye wivu ama tamaa kwa mtu huyo unaetamani kuwa kama yeye (Role Model). Japo kuwa na wivu ni asili ya kila mwanadamu lakini jifunze jinsi ya kuzuia hilo kutokea. Jaribu kutambua kila unaposikia wivu, hatua ya kwanza unapojitambua umeona wivu jaribu kusahau mara moja. Huwezi kufanana na mtu yeyote. Wewe unaweza kujiona una mapungufu na pia watu wanaokutazama kuna wanaopenda kuwa kama wewe. Jaribu kujikumbusha kuwa kila mtu amepangiwa maisha tofauti na yako na labda huyo unaemuonea wivu anatamani kuwa kama wewe. Sio kila mwenye mafanikio ameyapata kwa urahisi, bali wamepitia ama kufanya mambo mabaya kupita kiasi.
Jaribu kuwa na mipaka
Jaribu kuhakikisha unakuwa na mipaka na kujali yale muhimu katika maisha yako. Weka mipaka na angalia muda unao spend na watu. Hakikisha una mambo mengine ya kufanya katika maisha yako nje ya mahusiano uliyokuwa nayo, kama ni shule, kazi, marafiki, kwenda kwenye mazoezi au familia yako. Kuwa na mipaka na kila mtu na wasiliana nao pale unapowaitaji na si kila wakati, hii itakusaidia kuwa na maisha yako binafsi.
Simama kwa miguu yako
Kama wewe ni mwanaume ama mwanamke, unatakiwa kujifunza kusimama kwa miguu yako, hii itakusaidia kwa watu wengine kutokuchukua nafasi ya matatizo yako kama mtaji. Jifunze jinsi ya kusema hapana. Jaribu kuishi maisha ya kujitegemea na si ya kutegemea kusaidiwa na watu. Tafuta kazi ama shuguli yoyote itakayokuingizia kipato. Unapokuwa na tatizo jaribu kutafakari suluhisho la tatizo lako na si kusubiri rafiki jamaa ama ndugu kukusaidia kuamua ama kuchukua hatua.
Jifunze kusema hapana
Jiweke wewe mbele kwanza badala ya kuweka watu wengine kwanza. Kwa mfano mtu anakuomba umkopeshe pesa, si lazima umkubalie kila mtu. Hata kama rafiki yako atataka kukuazima gari mueleze gari halipo tena. Usijaribu kuwa mzuri kwa kila mtu. Jaribu kujifunza kusema hapana kwasababu kuna watu watatumia mwanya wa wewe kutokuwa na mamlaka na kilicho chako kwa manufaa yao binafsi.
Jiamini
Utakapojiamini kwamba unaweza na una ujaribu, utakuwa na ujasiri mkubwa sana. Timiza malengo yako na kile unachokitaka. Unapokosa kujiamini ama unakaribia kuwa mtu wa namna hiyo, utafanya watu wakutumie kutimiza malengo yao badala ya wewe kutimiza malengo yako.
Fanya watu wako wa karibu wafahamu pale wanapokukera ama kukukwaza
Kama mtu amekukwaza kwa njia yoyote ile, hakikisha unamfahamisha. Wakati mwingine inakuwa vigumu kuonyesha unavyojisikia hasa unapokuwa na hasira. Lakini kwa kumwambia mtu unavyojisikia itakusaidi kuzuia mtu kukukwaza ama kukukasirisha tena. Jaribu kuepuka kuzungumza na mtu pale unapokuwa na hasira kali. Kwani hiyo itapelekea kuzungumza maneno ambayo hayatatengeneza bali yataharibu. Kuwa na subira na zungumza na aliyekuwaza pale hasira yako itakapokuwa imetulia.
Subscribe to:
Posts (Atom)