Kuishi mijini kuna mazuri na changamoto zake, Uzuri kwamba kuna maisha mazuri na kujifunza mambo mengi zaidi kutokana na maendeleo ya eneo unaloishi. Pamoja na uzuri huo pia kuna changamoto zake ikiwemo ugumu wa maisha. Vijijini kuna changamoto ya ugumu wa maisha lakini mjini changamoto hii ni kubwa zaidi. Katika changamoto za kuishi mjini ni pamoja na garama za juu za chakula. malazi pamoja na mavazi. Na kutokana na ugumu wa maisha na garama za juu za chakula, mavazi na malazi mijini kunafanya watu kufunguka akili na kujua jinsi ya kupambana na changamoto hizi. Na kihi ndicho kilichonifanya mimi kuwaza sana na kufikiri hili jambo ninalotaka kulielezea hapa.
leo hii nimegundua kwamba tuna njia nyingi sana za kupambana na ugumu wa maisha. Katika maisha ya kila siku tunatumia garama nyingi sana kwenye chakula na malazi. Na kwa sababu hiyo inatulazimu kutafuta ama kuishi katika nyumba zenye maeneo madogo na hayana nafasi maalum ya kuzalisha chakula kitakacoweza kukimu mahitaji ya familia. Lakini hii tusiione kama changamoto kwani kuna njia nyingi sana ya kuzalisha vyakula vya kukimu familia zetu hata kwa yale maeneo madogo tunayoishi. Hii ni kwa kutumia makopo ama chupa za plastic kwa kukuza mboga za majani katika uwa mdogo wa nyumba yako.
Nafasi ndogo nyumbani kwako isiwe sababu ya wewe kutumia garama kubwa kununua mboga na viungo vya chakula nyumbani kwako. Kwa nafasi ndogo uliyonayo una uwezo wa kuhakikisha unapunguza garama za maisha za kununua chakula. Hii ni kwa kuhakikisha unatafuta makopo ama chupa za plastiki zilizokwisha kutumika kama nilivyoonyesha kwenye picha hizi. tafuta udongo mzuri na kama utapata mbolea ya kuku itakuwa ni vizuri zaidi. Hii ni kwasababu mbolea ya kuku haina takataka zinazoweza kusababisha kuota magugu ama majani yasiyohitajika kwenye makopo yako. Unaweza pia kutumia mbolea ya ng'ombe ila uwe tayari kung'oa magugu kwenye chupa zako kila wakati. Hii ni kwasababu Ng'ombe hula majani na matunda ya aina mbalimbali na kuyatoa kwenye kinyesi yakiwa hai ama kuwa na uwezo wa kuota tena. Unaweza kuchanganya udongo wako na mbolea ya kuku pembeni ka kuuacha kwa wiki moja ili ujichanganye vizuri na kasha kuujaza kwenye makopo yako tayari kwa kusia mbegu ama kupanda miche ya mboga na matunda unayoyahitaji katika uwa mdogo wa nyumba yako.
Siwezi kuacha kusema kwamba uzalishaji huu una manufaa makubwa na msaada mkubwa kwa familia. Uzalishaji huu wa mboga za majani utapunguza garama kubwa za maisha yako na pia familia yako itajipatia lishe bora. Zoezi hili ni zuri kwa sababu unalinda mazingira kwa kuhakikisha makopo ya plastic yanahifadhiwa vizuri na kuzalisha chakula kwa familia, kwani kwa kutumia makopo mia ya plastiki una uwezo wa kilisha familia yako mwaka mzima chakula bora kwa garama kidogo. Hii inawezekana kwa kutengeneza frame ndogo kwenye uwa wako na kutengeneza nafasi ya kuhifadhi maji utakayoyatumia kumwagia mimea yako kuifadhiwa na kutumika baadae. Uzalishaji huu wa mboga za majani unahifadhi si eneo tu bali unahifadhi pia maji kutopotea ardhini bali kubaki katika eneo ulilotenga chini ya fremu yako ya mbao na kutumia tena kumwagilia mimea siku inayofuata. Kiufupi ukulima huu unatumia nafasi ndogo, garama kidogo, kuhifadhi maji na kuipa familia yakko chakula bora na afya bora. Mimi nimechukua hatua kwa kufanya hivi nyumbani kwangu, na wewe chukua hatua na utaona umuhimu wa hili ili kupunguza njaa majumbani mwetu.
Chupa za soda kubwa zilizotumika kuotesha vitunguu