Maishafrika Adventure for the best Safari in East Africa

Thursday, February 18, 2016

SO YOU WANT TO BE YOUR OWN BOSS?

 

 
So You Want to Be Your Own Boss?
 
 

Kama unataka kuanza biashara na hujui pa kuanzia, usihofu, haupo peke yako. Watu wengi wanapenda kufanya kazi wanazo zipenda, na zile zitakazo wawezesha kutimiza malengo yao. Usijali lolote cha muhimu ni kuhakikisha unakuwa bosi wako mwenyewe, na hii unaweza kuanza leo hii unaposoma hii blog.
Yafuatayo ni mambo yanayoweza kukusaidia kutimiza malengo yako;
Jithaminishe uwezo wako na hakikisha unajiamini kuwa ni wewe tu utakae timiza lengo hili. Je unatakiwa kulaumu uchumi? muajiri wako, mpenzi wako ama familia yako?  Mabadiliko yanaweza kutokea tu kama utachukua maamuzi magumu.
Chagua biashara nzuri utakayo iweza. Jipe ruhusa ya kupambanua mambo. Kuwa huru kuangalia mambo tofauti yanayokuzunguka. Angalia muonekano wako, staili ya maisha ya jamii iliyokuzunguka na umri wa jamii inayokuzunguka. Mara nyingi hatukubaliani na hili lakini ni jambo muhimu sana katika kutimiza ndoto hii. Jiulize ni nini kitakupa nguvu hata pale utakapokuwa umechoka.
Kuna mambo matatu yatakusaidia kujua biashara unayoifanya ni sahihi.
Siku zote fanya biashara unayoijua, angalia muda uliokuwa ukifanya kazi kwa muajiri wako na fikiria utaalamu huo ukiufanya kwenye biashara yako itakuwaje.
Jaribu kufanya kile wengine wanachokifanya, jifunze kupitia biashara inayofanana na ya kwako. Na hapo utatambua kama ndiyo biashara unayoifahamu na usisite kuanza.Jaribu kutafuta suluhisho ya changamoto unayofikiria yanaweza kutokea katika biashara hiyo baada ya uchunguzi. Je kuna nafasi kwenye soko? Je huduma ama bidhaa unayotaka kutoa inahitajika katika soko sana? kama jibu ni ndiyo ingiza bidhaa hiyo ama huduma hiyo. Hakikisha unapochukua maamuzi unajitolea kujifunza na kupata uzoefu kabla ya kuanza kutumia mtaji wako.
Hakikisha unatengeneza mchanganuo wa biashara ili kukuwezesha kufanikiwa.
Watu wengi hawapendi kutengeneza mchanganuo wa biashara (Business plan), lakini itakusaidia kulifikia soko mapema. Mchanganuo wa biashara utakusaidia kuiweka sawa biashara yako, kujiamini na kufikia malengo. Mchanganuo wako hautakiwi kuzidi upande mmoja wa karatasi. Unatakiwa kuandika malengo, mategemeo na vitendo hatua kwa hatua, na biashara yako itakuwa kubwa.
Jiulize maswali yafuatayo:
Ninajenga nini?
nitamuhudumia nani?
Ninatoa ahadi gani kwa wateja wangu/na kwangu mimi mwenyewe?
Malengo yangu ni nini, mipangilio na hatua ntakazo piga kufikia malengo yangu?
Jua kundi unalolihitaji kufanya nao bishara kabla hujagarimia chochote

Kabla hujaanza kugarimia biashara, jaribu kafuatilia kama watu watakuwa tayari kununua bidhaa ama huduma unayotaka kuitoa. Hili ni jambo la muhimu sana kulifanyia kazi. Unaweza kulifanya hili kwa kulinganisha soko lako la biashara unayotaka kuifanya. Kwa maneno mengine ni nani haswa atanunua bidha au huduma yako zaidi ya familia na rafiki zako? ( Na usiseme kilamtu Tanzania hii anahitaji huduma unayoitoa, "Niamini hakuna kitu kama hicho") jaribu kufikiria ukubwa wa watu unao walenga? Wateja wako ni kina nani? Je bidhaa yako ama huduma yako ni ya muhimu sana katika maisha yao ya kila siku? na ni kwanini wanaihitaji?
Angalia kipato chako na chagua njia sahihi ya kupata fedha unazozihitaji katika biashara yako. Kama mjasiriamali, maisha yako binafsi yanachangia katika  hili. Una uwezo wa kuwa mmoja kati ya wawekezaji wakubwa. Hivyo unatakiwa kuwa na uelewa mkubwa wa kipato chako halisi, na uwezekano wa kutafuta kipato hicho, ni hatua muhimu ya kwanza kabla ya kutafuta mtaji nje wa biashara yako. Hili ni muhimu ndiyo sababu ya kusisitiza kwenye post zangu zilizopita kwamba tunatakiwa kujifunza kujiwekea akiba. Ukiwa unatengeneza mchanganuo wa biashara, unatakiwa kulipa uzito swala la mtaji kutokana na biashara unayotaka kuifanya, kutegemeana na eneo unalotaka kufanyia biashara. Ni muhimu kuhakikisha una mtaji wa kuanzisha biashara yako, na ni muhimu kufahamu aina ya fedha utakazokubali zitumike katika biashara yako ( kwa mfano kupokea fedha za nje, Credit Card, etc), ni lazima ukubaliane na haya katika kukuza biashara yako.
Jenga mtandao
Ukisha jenga malengo ya biashara yako, unahitajika kujenga mtandao wa watakao kuunga mkono, washauri, wawekezaji wenzako, watakao kupa huduma na watakao tembeza ama kuitangaza biashara yako. Kama utaiamini biashara yako na wengine wataiamini pia.
Jenga mitandao kitaifa na kimataifa, na kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram, Face book, Twitter, n.k na kwenye magroup mengine ya kibiashara.  

Uza bidhaa ama huduma yako kutokana na thamani yake. Hata kama tunanunua na kuuza bidhaa ama huduma kila siku,  watu hawataki kuuziwa vitu bei gali, jaribu kusaidia watu kwa kuuza bai stahili. Jinsi unavyotoa huduma kwa watu wengi, unaongeza mauzo na idadi ya kipato chako. kama ni mjasiriamali unaemjali mteja wako lazima utajiuliza maswali yafuatayo:
Je ninaweza kuwapa  nini?
Je nitafanyaje ili waridhike na huduma ama biashara ninayo ifanya kwao?
Haya maswali mawili yatakusaidia kukuongoza kwenye njia mpya katika bidhaa yako ama huduma yako na kuiongezea thamani, ambayo wateja wako wataridhika.
Kuwa tayari kusema wewe ni nani, na unafanya nini bila kuwa na uwoga. Hakikisha unafanya hivyo kwenye Mitandao ya kijamii, ili kujitangaza na kuitangazia dunia.
Jaribu kufanya kile unachodhani kitafurahisha followers wa biashara yako.

Pamoja na kwamba mitandao ya kijamii ina umuhimu kwa sasa ni muhimu kuitumia, na pia sisite kutumia njia nyingi za kutangaza biashara yako, kama kwenda kueleza watu wewe mwenyewe kuhusu bidhaa ama huduma unayoitoa, website, blog post, speech, news latter, simu n.k. Kama utafuata hatua hizo hapo juu, utakuwa vizuri na utakuwa njiani kuwa bosi wako wewe mwenyewe. ni muhimu kukumbuka haupo peke yako. Kama unataka kuwa bosi wako mwenyewe lakini unaona umekwama, jiunge na wajasiriamali wengine kwa nia tofauti. Utashangaa kupata habari za wajasiria mali walio fanikiwa wakieleza mapito yao magumu kufika hapo walipofika na itakuwa ni njia nzuri ya mawasiliano yatakayokuwa ni chachu katika biashara yako na utagundua mafanikio yako yapo katika  pingili za viganja vya mikono yako.
Ndoto yangu ya kuwa my own boss ni hiyo picha hapo juu, Ninafanya kazi kwa bidii sana kuhakikisha naitimiza, ninasali sana na ninaweka akiba ipasavyo kuhakikisha natimiza lengo langu hilo. "Lets work hard, lets save money, lets achieve our goals. Lets work hard and pay our bills". "My dream business in coming years" "Pergola .....!!!"
 

Monday, February 8, 2016

NINI CHA KUFANYA X WA MPENZI WAKO ANAPOKUSUMBUA






Tumekuwa tukisikia ama kupitia kwenye mahusiano yanayohusisha vurugu na utomvu wa nidhamu wa wapenzi wa zamani, ambao hawako tayari kumwacha mpenzi wako.  Labda anafikiri kuna uwezekano wanaweza kurudiana ama anataka kukukwaza wewe mpenzi wa sasa kwenye mahusiano yenu kwa sababu ya wivu uliopitiliza. kwa sababu yoyote ile, Ni vigumu kuishi maisha ya furaha, ukiwa katika mahusiano mapya na wakati huohuo mpenzi ama wapenzi wake wa zamani wanamfuatilia mpenzi wako ni jambo gumu na la kukera.

Lakini kuna jambo moja, tunatakiwa kukumbuka kwamba "wazimu" wa mpenzi wa zamani unasababishwa na kupitia katika wakati mgumu (emotion), na yeye ni binadamu pia lazima apitie hilo, ila anajaribu kutatua wakati wake mgumu kwa njia zisizo faa. Kufanya mambo yaende vizuri, unatakiwa wewe kuwa na busara. Kama unataka akuache wewe na mpenzi wako muishi maisha yenu kwa roho safi, kuna mambo unatakiwa kuyafanya;

Jaribu kuchukua nafasi yake
Najua hii ni ngumu kwasababu huyu ni mwanamke ama mwanaume anaekusumbua, lakini kwa muda mfupi jifikirie ingekuwa ni wewe ungejisikiaje. Hebu fikiria anajisikiaje: Ni moja kwa moja anafanya hivi kwasababu ameumia moyoni mwake na hakuwa tayari kuachana na mpenzi wake. Ndiyo anajaribu kutatua hili kwa njia isiyo sahihi , na ndiyo si mtu mzuri kwako, lakini kama mwanadamu unatakiwa kuwa mtu mwema kwake. Amekwazika ndiyo sababu ya konyesha tabia zisizo za kawaida. Jifikirie utajisikiaje baada ya kuachana na mpenzi wako, na kumuona mpezi wako na mpenzi mwingine na wewe bado unampenda. Inaumiza na hiyo inaweza kuwa ni sababu ya yeye kuwa na tabia hizo.


Jaribu  kumkwepa
Kabla ya kufanya lolote, jaribu kadiri ya uwezo wako kumkwepa. Wakati mwingine, kukwepa mtu anaejaribu kukukwaza ama kukukasirisha ni njia nzuri ama kutatua tatizo. Kwa kufanya hivi unamuonyesha hujali, na una mambo muhimu ya kufanya zaidi ya kumfikiria yeye. Jaribu kuishi kama hakuna lolote linaloendelea na endelea na maisha yako ya kila siku. usipokee simu zako wala kujibu meseji zake kwasababu huna la kujadili na yeye. Kama ataendelea kukusumbua ni vizuti kumblock kwenye mitandao ya jamii ama simu. Epuka kuwa karibu na marafiki zake ama watu wake wa karibu. Epuka kuzumgumza habari zake wala kufuatilia habari zake. Kama ushauri huu haufanyi kazi endelea kusoma ushauri unaoendelea.

Zungumza na mwenza wako kuhusu hili
Kama utajaribu kuyafanya hayo hapo juu na bado ataendelea kukusumbua, unatakiwa kuzungumza na mwenzi wako kuhusu linaloendelea. Mueleze ni jinsi gani mpenzi wake wa zamani anavyokufanyia na mueleze kwamba unakwazika sana na vitendo vyake. Kuwa muwazi kwake na mueleze hili kama wapenzi, ili mlitafutie ufumbuzi kama wapenzi. Anatakiwa kufahamu unavyojisikia kutokana na matendo ya mpenzi wake wa zamani.

Epuka kuharibu mambo
Najua kuna wakati unajaribu kufanya vitendo vitakavyomfanya mpenzi wake wa zamani apate wivu ili asiwasumbue tena. Utataka kupost picha ukiwa mmekumbatiana, mnapigana mabusu kwenye mitandao ya kijamii ambayo una uhakika ataziona, na wakati mwingine unaweka status kama "Nakupenda sana, hana muda na wewe tena",   usijaribu. Huku ni kujiweka madoa mwenyewe. Kufanya vitendo kama hivi, ni kumuongezea hasira na hujui at react vipi. Hili litafanya hali iwe mbaya zaidi. Jaribu kutumia busara zaidi na hekima.

Mwambie Mwenzi wako azungumze naye
Kama mambo yanaendelea kuwa mabaya na yamekushinda kabisa, zungumza na mwenzi wako na mwambie anatakiwa kuzungumza na mpenzi wake wa zamani, kabla wewe hujazungumza nae lolote. Hii ni kwasababu yeye ndiye aliyekuwa na mahusiano naye na sisi wewe. Mueleze jinsi unavyojisikia na asipolifanyia kazi litakuja kuathiri hadi mahusiano yenu. Mwambie azungumze naye na amueleze anatakiwa kuacha vitendo vyake anavyo kufanyia na amueleze aelewe.

Usijaribu kupigana naye
Usajaribu kutatua hili tatizo kwa mikono yako, Usipigane naye wala kupambana naye kwa maneno makali kwenye mitandao ya jamii. Hili halitakusaidia bali litafanya mambo yawe mabaya zaidi na litaongeza shid zaidi.

Zungumza naye kiutu uzima zaidi
Badala ya kupambana, jaribu kusuluhisha hili tatizo kiutu uzima zaidi. Muuliza kama mnaweza kuonana ili mzungumze,. Au mtumie meseji kwenye Face book, na ujumbe huo usiwe wa kumtisha, kumlaani ama kumuonya. Kuwa muwazi kwake na mueleze upendi mambo anayoyafanya, uko very happy kwenye mahusiano yako na na utafurahi kama ataendelea na maisha yake na kuachana na nyinyi. Kuwa mwenye busara na jaribu kuzungumza nae kwa upendo na hakikisha ujumbe kauelewa. Hili litasaidia kumfanya atambue kuwa anatakiwa kuacha upuuzi. Kumbuka hili ni suluhisho la mwisho kabisa kama umejaribu kila njia na ikashindikana. Tuepuke vita juu ya mahusiano kwasababu haina tija yoyote.








Wednesday, February 3, 2016

JINSI YA KUCHAGUA KUWA NA FURAHA MAISHANI MWAKO



Katika maisha yako ni wewe tu ndiye utakae chagua kuwa na furaha. Kuwa na furaha ama kutokuwa na furaha ni chaguo lako. Kwa kila wakati utakaokuwa una hasira ama kukasirika unapoteza sekunde 60 ya furaha. Kuwa na furaha wakati wote, na kama watu hawataki kukuona na furaha, usiwajali. Maisha si ya kumnyenyekea kila mtu.

Kama unauwezo wa kujijua kama unaogopa, unafurahi , una unwezo wa kusimama na kuongea lolote hata kama sauti yako inaonyesha uoga, kujiamini na kuomba msaada pale unapo hitaji, na ujasiri wa kukubali msaada pale unapouhitaji, bila shaka una kila sababu ya kuwa ni mtu mwenye furaha kila wakati.

Simama leo hii na chukua maaumuzi ya kuwa ni mtu mwenye furaha
Chagua kuwa bora kuliko unavyodhani
Jipe nafasi ya kufanya kila unachoweza, Kuwa na malengo ya maisha yako na hakikisha unakuwa commited kuhakikisha unatimiza malengo  yako bila kuruhusu changamoto zozote. Epuka kufananisha maisha yako na ya mtu yeyote. Kujiwekea malengo (Goals) na kutimiza malengo yako ni kati ya vitu vitakavyokufanya uwe na furaha. Hii itakuonyesha kwamba wewe ni mtu ambaye una malengo na una uwezo wa kutimiza malengo yako kwa wakati muafaka. Ila swala la muhimu zaidi ni kuepuka kujaribu kuwa kama mtu Fulani, ila usiache kujaribu kuwa zaidi ya watu wanavyofikiri. Na kama unataka kufanana na mtu jaribu kujifananisha na wewe mwenyewe ulivyokuwa kabla ya hapo ulipo. Wewe mwenyewe ndiyo mfano wako na siku zako utakuwa wewe na si mtu mwingine.

Chagua kuwa na marafiki ama watu wenye mwenenda mwema
Jaribu kutumia muda wako kuwa na marafiki ama watu wema na wenye busara. Marafiki ama mahusiano ya aina yoyote yanatakiwa kukusaidia na si kukuumiza. Kuwa na marafiki ama mahusiano na watu watakaokusaidia kutimiza malengo yako. Chagua marafiki watakaokufanya ufurahi kwa kuwajua na si kujuta kuwafahamu. Life is too short to spend time with people who suck the happiness out of you. Utakapojitoa kwenye urafiki na watu wasiofaa, itakusaidia kutambua kwamba unastahili kuishi maisha yako, na kuishi maisha yako ndiyo maisha ya kweli.

Focus na kile ulicho nacho, na si kile usichonacho
Unaposhukuru kwa kile ulichonacho unaonyesha kwamba hata kile kidogo ulichonacho kina thamani. hii itakusaidia kuwa ni mtu mwenye furaha, kwasababu umeridhika na kile ulichonacho na huta sononeka kwasababu mtu Fulani anacho na wewe huna. Lazima umshukuru mungu kwa kile alichokupa kwasababu kuna wengine walitaka kufika ulipofika lakini hawakuweza kwasababu tofauti.

Chagua kuwa na tabia nzuri
Kinachosababisha wakati mwingine kutokuwa na furaha ni kuwa na picha Fulani kwenye vichwa vyetu.Na sababu kubwa inayosababisha wengi wetu kukata tama ni kuangalia umbali tunaotaka kwenda badala ya kuangali tulipotoka. Kumbuka maisha ni safari ndefu sana na si makao kamili. Kila kinachotokea katika maisha ya kila siku ni zawadi na ni opportunity ya maisha. Kubaliana na yaliyotokea, tabasamu na likubali kama lilivyo. Ukikubali kwamba yaliyojiri leo ni bora then maisha yako yatakuwa bora kila siku. Siku zote tabia nzuri huleta matokeo mazuri.

Tabasamu kila wakati
Kutabasamu ni chaguo lako, na si miujiza. Usisubiri watu watabasamu, watu wanatakiwa kujifunza kutoka kwako jinsi ya kutabasamu.Tabasamu lako linaweza kufanya watu wa karibu yako kutabasamu pia. Tabasamu lako dogo kawaida hutuma ujumbe kwenye ubongo wako kwamba una furaha. Kwa wewe kutabasamu kila wakati kuna kufanya uwe ni mtu mwenye furaha.


Kuwa muwazi
Jaribu kuwa muwazi kwako mwenyewe na kwa kila mtu. Usiwe muongo na usie aminika bali kuwa muaminifu na mkarimu, fanya matendo mazuri na hii inapunguza ugumu wa kuishi na watu na maisha yako mwenyewe. unapovunja sharia ama masharti Fulani inakaribisha changamoto nyingi katika maisha yako ya kila siku. Fanya maisha yako kuwa simple sana na enjoy kila unachokifanya ambacho kiko sawa. Jaribu kuepuka drama zitakazo sababisha matatizo na madhara katika maisha yako.

Toa masaada pale inapowezekana
Jali watu, katika maisha utalipwa kwa yale mema uliyoyafanya. Unapotoa msaada kwa mtu anaehitaji msaada, mungu anakubariki katika maisha yako pia. Jaribu kufanya kitu kilicho juu ya uwezo wako, hasa katika kutoa msaada kutamfanya unaempa msaada afurahi na wewe kupunguza matatizo pia. Makosa makubwa tunayoyafanya ni kutoa misaada kwa watu wasiohitaji misaada na badala ya kuwasaidia tunawafanya wawe wavivu wa kazi na wavivu wa kufikiria. Fanya uchunguzi n a utatambua watu wanaotoa msaada kwa wasiohitaji msaada hufanya hivyo ili waonekane na watu wengine, ama ufanya hivyo ili kumkomoa mtu mwingine. Badala ya mambo yao huwa magumu kwasababu mungu hajatambua wala hajaona faida ya msaada aliotoa. Tunatakiwa kujifunza kufanya jambo pale ambapo kuna uhitaji mkubwa.

Inapofikia wakati wa kuachana, usifikirie marambili ila fanya maamuzi sahihi
Wakati mwingine unatakiwa kuwa na msimamo na maamuzi ya maisha yako. Upendo unadhamani lakini si kwa ugomvi ama mapambano, na usikubali wewe kugombana kwasababu ya upendo ama mapenzi. Tambua kuwa si sawa wewe kuwa unapambana juu ya mapenzi, bali na wewe unatakiwa kugombaniwa pia. Kama hawaoni umuhimu wa upendo wako ama mapenzi yako unatakiwa kuachana naye (Move on) na kutambua uliwapenda zaidi ya wao walivyokupenda . Baadhi ya mahusiano na changamoto zake ni fundisho na hatua tosha katika maisha. Ukilazimisha kuwa na mpenzi ama kupenda mtu asiyekupenda mambo yako yatakuwa mabaya zaidi kwasababu utakosa furaha. Jaribu kuachana na watu wasiothamini pendo lako ni hilo litakufanya uwe na furaha zaidi.

Kuwa tayari kuvuka hatua nyingine katika maisha
Una chaguo la kuendelea kushikilia vikwazo katika maisha yako ama, kuachana na vitu vilivyokukwaza ili uwe ni mtu mwenye furaha. Usikubali mafanikio yakuumize kichwa na kutokuwa na mafanikio kuumize moyo wako. Kila kunapokucha ni siku mpya na ni mwisho wa siku iliyopita, likubali hilo na fanya kazi kwa bidii, tabasamu, na angalia mbele na si kuangalia jana ulishindwa wapi. Na usisahau kutabasamu hakumaanishi kila wakati una furaha, bali wakati mwingine ina maana rahisi, kuwa wewe ni shupavu na uko tayari kukabiliana na changamoto za kimaisha.

Na kumbuka, akili yako ni hifadhi yako binafsi, usiruhusu imani potofu unayoambiwa na watu wanaokuzunguka. Ngozi yako ndiyo mipaka ya maisha yako, usikubali mtu yeyote kuingia ndani yake. Linda na heshimu mipaka yako na yale unayokubali kuambiwa ama kufanyiwa na watu. You are a role model of your self, uhitaji kufanana na mtu mwingine kwasababu wewe ni wewe na hakuna anayefanana na wewe.

Usiruhusu mawazo ya mtu yoyote yakufanye ubadilishe maisha yako na kubadilisha nmuonekano wako. Usijitoe kafara kwa vile ulivyo kwa kuwa mtu mwingine anakutoa kasoro. Jipende kama ulivyo ndani na nje. Hakuna mwenye nguvu ya kukufanya wewe ujione huna thamani, labda kama wewe mwenyewe utaruhusu hilo.

Chaguo ni lako, chagua kuwa na furaha.