Hili swali limekuwa ni gumu na mtihani kwa watu wengi sana ambao ni waajiriwa wa sekta binafsi na wale walio ajiriwa kwenye mashirika ya umma. Na wengi wamekuwa wakipewa ushauri mbaya ama ushauri uliowakatisha tama. Leo ningependa kukwambia unaweza kuwa mjasiria mali bila kuacha kazi iliyokuwa ikikuingizia kipato kila mwezi. Una uwezo wa kuwa mjasiriamali na kuendelea kufurahia kazi unayoifanya kila siku bila kuaribu utaratibu wako wa kazi. Yafuatayo ni mambo matano muhimu yatakayokusaidia kufanikisha hili;
Ichukulie kazi yako kama ni Baraka kutoka kwa mungu.
kazi yako si mzigo mkubwa unaoubeba na unatamani siku moja uushushe. Kazi yako ndiyo inayokuwekea chakula mezani wewe na familia yako na pia ndiyo inayokufanya wewe kuheshimika katika jamii yako. Na pia kimbuka kazi yako ndiyo itakayokuwa muongozo ama mtaji wako katika biashara yoyote unayotegemea kuianzisha. Your job will make your entrepreneur dream come true. Mshahara wako utakuwa chanzo kikibwa cha wewe kuwa na nguvu ya kuchukua mkopo ama kuweka akiba ya kukuwezesha wewe kupata kianzio cha biashara ndogo unayotakiwa kuianzisha na si kuichukia ajira. Ajira yako ndiyo itakayo kunyanyua katika mipangilio yako yote ya ujasiria mali hadi pale utakapokuwa na mafanikio makubwa na una uwezo wa kuacha kazi na kusimamia biashara zako wewe mwenyewe. Kama biashara yako haijashamiri tafadhali epuka kuacha kazi na kwenda kusimamia biashara ambayo hujafahamu muelekeo wake.
Jali muda wako
Madhara ya kuwa kwenye ajira ukiwa ni mjasiriamali yapo na ni makubwa kiasi ambayo hukatisha tamaa watu wengi. Hilo lisikutishe wala kukusumbua, swala la muhimu ni kujipangia muda utakaofanya kazi na muda utakaotumia kwenye kazi zako za kijasiriamali. Jaribu kila muda unaoupata baada ya kazi unautumia katika kufanya shuguli zako za kijasiriamali. Sheria za kazi za umma ni kufanya kazi masaa nane ama tisa na katika sekta binafsi baadhi ni masaa hayohayo na mashirika mengina wanaongeza muda zaidi kwa makubaliano maalumu ama muda ni pungufu zaidi. Mara nyingi unapofanya kazi masaa tisa unakuwa na masaa si chini ya manne abla ya kulala ama kupumzisha mwili. Masaa manne ni muda mrefu sana kwa kusimamia kazi zako za ziada. Unaweza kuajiri mtu wa kuzifanya kazi hizo na wewe kutumia muda wako mchache kusimamia ama unaweza pia kuzifanya mwenyewe katika hayo masaa manne. Kwa mfano kilimo, unaweza kukifanya muda ambao upo nyumbani, ama ufugaji na biashara ndogondogo pia una uwezo wa kuzifanya mwenyewe kwa muda mfupi baada ya kazi. Ili kuwa mjasiriamali inabidi upunguze muda wa kufanya vitu ambavyo havikuingizii vipato na badala yake jaribu kufikiria na kujituma katika mambo yatakayokusaidia kukuingizia kipato cha ziada. Jaribu kuweka smart phone yako mbali na jaribu kuepuka kupoteza muda kwenye social media, jaribu pia kupunguza muda wa kulala na jiulize je muda ambao nipo free ninaweza kuutumiaje kujiongezea kipato. Kumbuka kila lisaa unalopoteza ni sawa na kupoteza kipato.
Chukua hatua kwa kila mpango ulionao.
Unapokuwa na malengo ya kuwa mjasiriamali ukiwa umeajiriwa, unatakiwa kuwa na malengo na kuhakikisha umefanikisha ndoto yako. Fikiria ni kitu gani kinaweza kukuongezea kipato na je mtaji wake utaupataje. Hili ni jambo la muhimu sana, hakikisha unafanya biashara ama shuguli itakayoendana na kipato chako na una uzoefu nayo na pia hakikisha unakuwa na uwezo wa kusimamia ipasavyo. Ni vigumusana kuanza biashara kubwa kuliko mtaji uliokuwa nao kwasababu biashara hiyo itakuwa ni ndoto isiyotimia. Hakikisha kama ni kuchukua mkopo, unachukua mkopo utakaoweza kuulipa na hata biashara itakapoenda vibaya ajira yako inaweza kulipa mkopo huo.
Ni kipi utakachokifanya tofauti na wenzako
Jaribu kufanya biashara tofauti na wenzako, usifanye biashara ambayo inafanana katika eneo moja. Na kama ni biashara inayofanana na wenzako hakikisha ya kwako una kitu tofauti na wanachokifanya wenzako. Hii itakusaidia kupata wateja wengi na mzunguka wa mtaji wako kwenda kwa haraka zaidi na kupelekea kipato chako kuongezeka kama ambavyo lilikuwa lengo la biashara.
Fanya ajira yako kuwa muongozo wa biashara yako
unapoamshwa na simu ama alarm clock asubuhi, usisikitike muda wa kazi umefika bali amka wahi kazini ili uwahi kutoka na kwenda kusimamia biashara zako. Kazi yako ndiyo ajira yako ya kwanza na biashara yako ndiyo ajira yako ya pili. Na usisahau ajira yako ndiyo muongozo wa biashara yako kwani ni moja ya kitu kinachokuongezea kipato ambacho ndiyo msingi wa biashara yako. Na kama ujasiriamali wako unaufanyia katika ofisi yako uliyoajiriwa tumia fursa vizuri bila kufaya uzembe wala kuvunja sharia za kazi na kuvuka mipaka ya kazi. Kumbuka ajira ni muhimu na ujasiria mali pia ni muhimu sana.